December 12, 2012

LIKOWAPI JUKUMU LA MALEZI KWA MTOTO GOSBERT NA NYAMBULI WALIOTUMBUIZA SIKU YA UHURU UWANJA WA TAIFA

Ukiangalia katika picha hii utawakumbuka watoto hawa Nyambuli Mganga (5) na Gozbert Bwere (3) kutoka mkoani Mara ambao walikuja jijini Dar es salaam na kikundi cha ngoma za asili kutoka mkoani humo, kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania Bara yaliyofanyika kwenye uwanja wa Uhuru, watoto hawa walitia fora sana mbele ya Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. Jakaya Kikwete na wageni mbalimbali kutoka nje na ndani ya nchi waliohudhuria katika maadhimisho hayo.

Shughuli kubwa iliyofanywa na mtoto mdogo Gozbert Bwere (3)katika upigaji wa ngoma ndiyo iliyowafanya baadhi ya viongozi wa kisiasa na Serikali kuenda kumtunza mtoto huyo, ambapo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa NEC CCM Nape Nnauye na Katibu Mwenezi wa chama hicho Mwigulu Nchemba walienda na kumtunza mtoto huyo kwa umahiri wake katika kupiga ngoma.
 
Katika pita pita za kusaka habari  maeneo ya Manzese katika moja ya kiota cha siku nyingi Frieds Coner na kumkuta mmoja wa wanakikundi akiwa na watoto hao nje ya hoteli hiyo, akajitambulisha kwamba yeye ni Mpalala Mwendwa na ni msaidizi wa Afisa Utamaduni wa Mkoa wa Mara akaongeza na kusema yeye amefuatana na kikundi hicho kama mmoja wa viongozi wa msafara kutoka mkoani Mara.

Chakusikitisha sana ni kiongozi huyo kuonekana akiwa ameshika chupa inayodhaniwa kuwa na pombe kali  akionekana kuwanywesha watoto hao pombe hiyo kwa kifuniko , huku mtoto Gozbert Bwere akikunja sura mara baada ya kunywa  ikiwa ni kuashiria kwamba hawezi kumudu kilevi.

Kitu kilichiniumiza sana nilipoongea na Bwana Mpalala Mwendwa aliniamba kuwa wazazi wa watoto hao wamebaki Musoma. Hivyo watoto hao wako chini ya uangalizi wa kikundi hicho pekee jambo ambalo si jema na kuna uwezekano mkubwa wa kumomonyoka kwa maadili ya watoto hao, kwani hawana ulinzi wa kotosha kama ilivyoshuhudiwa jana wakiwa wananyweshwa pombe na kiongozi huyo.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa NEC CCM Nape Nnauye na Katibu Mwenezi wa chama hicho Mwigulu Nchemba wakirejea jukwaani mara baada ya kuwatunza watoto hao Nyambuli na Gozbert wakati wakicheza ngoma katika maadhimisho ya miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania Bara kwenye uwanja wa Uhuru.
Mtoto Gozbert Bwere (3) akionyesha uwezo wake katika kupiga ngoma huku akiwa amelala chini katika maadhimisho hayo.
Mtoto Gozbert Bwere (3) akifanya vitu vyake katika kupiga ngoma katika maadhimisho hayo. (Na  FULLSHANGWEBLOG.COM)

No comments:

Post a Comment