Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
akimpokea mgeni wake, Rais wa Madagascar , Mheshimiwa Andry Rajoelina
mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere, Dar es Salaam leo, Ijumaa, Desemba 14, 2012 kwa ziara ya siku
mbili nchini.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
akiwa katika mazungumzo na Mgeni wake,Rais wa Madagascar , Mheshimiwa
Andry Rajoelina mara baada ya kuwasili nchini leo.
*******
Rais
wa Madagascar, Mheshimiwa Andry Rajoelina amewasili mjini Dar Es Salaam
mchana wa leo, Ijumaa, Desemba 14 kwa ziara ya kikazi ya siku mbili
nchini.
Kwenye
Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere mjini Dar Es Salaam ambako ndege
iliyomleta Rais Rajoelina ilitua saa sita na dakika 45 mchana, amelakiwa
na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa
Jakaya Mrisho Kikwete.
Rais Kikwete na Rais Rajoelina wamekula chakula cha mchana na wanatarajiwa kuanza mazungumzo rasmi baadaye leo.
Rais
Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa Tume ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya
Jumuia ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) amepewa jukumu na viongozi
wenzake ndani ya Jumuia hiyo kukutana na viongozi wa Madagascar
kuwalezea maamuzi ya mkutano wa viongozi hao wa SADC uliofanyika
mwishoni mwa wiki mjini Dar Es Salaam.
Rais
Kikwete tayari amekutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Marc
Ravalomanana, kiongozi wa zamani wa Madagascar aliyeondolewa madarakani
na Rajoelina.
Kwenye
mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Ikulu, Dar Es Salaam,
mwanzoni mwa wiki hii, Mheshimiwa Ravalomanana alithibitisha kuwa
amekubaliana na maamuzi ya viongozi wa SADC.
Miongoni
mwa mambo mengine, viongozi hao wa SADC wanataka viongozi hao wawili wa
Madagascar washawishiwe na wakubali kutogombea katika Uchaguzi Mkuu
uliopangwa kufanyika nchini humo mwakani.
No comments:
Post a Comment