Mwanamuziki
kutoka nchini DRC-Congo,Koffi Olomide akitia saini moja ya bango lenye
kampeni inayowatahadharisha madereva wa magari kunywa pombe
kupindukia,ikiwa ni hatari kwa afya na usalama wao kwa ujumla,pichani
kulia ni Mkurugenzi wa kampuni ya bia ya Serengeti,Bwa.Steve Gannon
akishuhudia tukio hilo,aidha katika tukio hilo Wanahabari mbalimbali
walishuhudia tukio hilo ndani ya hotel ya Serena Inn mapema leo
mchana.Koffi Olomide na skwadi lake la Quartie Latin wametua jana jijini
Dar kwa ajili ya maonesho yao mawili yatakayofanyika jijini Dar ndani
ya viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni siku ya jumamosi na jijini Mwanza
kwenye uwanja wa CCM-Kirumba siku ya jumapili kwa udhamini mkubwa wa
kampuni ya SBL kupitia bia yake ya Tusker Lager.
Bango alilotia wino Koffi Olomide.
Koffi Olomide akitoa vionjo vya moja ya wimbo wake mbele ya wanahabari,kulia kwake ni Mkurugenzi wa Mahusiano Serengeti Breweries,Nandi Mwiyombela akinogesha
Mkurugenzi
wa Masoko kampuni ya SBL,Ephraim Mafuru akiuzumguza mbele ya Wanahabari
mapema leo ndani ya hotel ya Serena Inn,kuhusiana na onesho la
Mwanamuziki kutoka DRC-Congo,Koffi Olomide linalotarajiwa kufanyika
kesho jumamosi kwenye viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar.
Baadhi ya wafanyakazi wa SBL wakifurahia jambo
Mkurugenzi
wa Mahusiano Serengeti Breweries,Nandi Mwiyombela akiwakaribisha wageni
mbalimbali wakiwemo wanahabari kwenye mkutano uliohusu onesho la
Mwanamuziki Koffi Olomide,ambalo limedhaminiwa na kampuni ya SBL kupitia
kinywaji chake cha Tusker.
Mwanamuziki
kutoka nchini DRC-Congo,Koffi Olomide akifafanua jambo mapema leo
alipokuwa akizungumza na wanahabari (hawapo pichani),ndani ya hotel ya
Serena kuhusiana na onesho lake atakalolifanya hapo kesho ndani ya
viwanja vya Lidaz Club,Koffi amewaomba washabiki na wapenzi wake waje
wajionee kazi kubwa atakayokuwa akiifanya jukwaani akiwa na vipaji vipya
kabisa katika tasnia ya muziki wa dansi nchini Congo.
Mkurugenzi
wa kampuni ya bia ya Serengeti,Bwa.Steve Gannon akimkaribisha Koffi
Olomide (hayupo pichani) na pia aliwataka mashabiki na wapenzi wa
mwanamuziki huyo wajitokeze kwa wingi na kushuhudia tukio hilo adhimu
hapo kesho.
Mkurugenzi
wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga akiwashukuru Wadhamini wa onesho la
Koffi Olomide pamoja na Wanahabari kwa ushirikiano mkubwa walioutoa
katika kuhakikisha jamii inapata taarifa mbalimbali kuhusiana na ujio wa
mwanamuziki huyo pamoja na onesho lenyewe.
Mkurugenzi wa Masoko kampuni ya SBL,Ephraim Mafuru akisalimiana mkono na Mwanamuziki wa Kimataifa Koffi Olomide.
Mkurugenzi
wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga pichani shoto akiwa ameambata na
mgeni wake Koffi Olomide sambamba na Mkurugenzi wa SBL,Steve Gannon
wakiwasili ndani ya ukumbi wa mikutano,Serena Hotel kwa ajili ya
kuzungumza na Wanahabari kuhusiana na onesho litakalofanyika kesho
kwenye viwannja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar
No comments:
Post a Comment