Na Hamisi
Mohamedi- Morogoro
Waziri wa mawasiliano nchini
Prof.Makame Mbarawa amefungua kikao cha pili cha mamlaka ya mawasiliano nchini
TCRA kilichofanyika jijini Dar es salam.
Akizungumza katika ufunguzi huo
Prof. Mbarawa amesema serikali imejipanga vyema katika kukabiliana na mabadiliko
ya kutoka katika mfumo wa Analogy na kwenda Digital.
Prof. Mbarawa amewataka mawakala
walioidhinishwa na mamlaka hiyo ya mawasiliano nchini TCRA wazingatie ubora wa
matangazo kama inavyotarajiwa na wengi.
Pia kwaupande wa wamiliki wa
nyombo vya habari Pro. Mbarawa amewataka wamiliki hao kujikita katika
kutayarisha vipindi vya kuelimisha jamii hasa jamii ilioko
vijijini ambayo ndio kundi kubwa la
watanzania wapo huko.
Mkutano huo wa siku mbili ulikuwa
na lengo lakuwakumbusha wamiliki wa vyombo vya habari na waandaaji wa vipindi
waandae vipindi vya kuielimisha jamii
No comments:
Post a Comment