December 08, 2012

MKE WA RAIS KIKWETE AFURAHIA MWISHO WA MWAKA NA WATOTO YATIMA

 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,(WAMA,) akiwapungia mkono watoto yatima (hawapo pichani) walihudhuria sherehe ya mwisho wa mwaka iliyofanyika kwenye viwanja vya Taasisi hiyo karibu na Ikulu jijini Dar, leo.
 Baadhi ya watoto yatima wakipata chakula cha mchana walichoandaliwa na Mama Salma Kikwete.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Twiga Cement Bwana Pascal Lesoinne mara baada ya sherehe ya mwisho wa mwaka waliyowaandalia watoto yatima kwenye ofisi za WAMA, leo.
 Mama Salma, akicheza na mmoja kati ya watoto waliohudhuria hafla hiyo leo.
Mke wa Rais na Mweyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akishirikiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Saruji ya Twiga Bwana Pascal Lesoinne kugawa zawadi mbalimbali kwa watoto yatima wanaolelewa katika baadhi ya vituo vya Dar es Salaam katika sherehe iliyofanyika kwenye ofisi za WAMA.

No comments:

Post a Comment