Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akihutubia
muda mfupi kabla ya kuanza kwa harambee ya kuchangia ujenzi wa
Kanisa la Lutherani usharika wa Akyeri,Dayosisi ya Meru Mkoani Arusha.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa
akipokelewa na viongozi wa Kanisa la Lutherani usharika wa
Akyeri,Dayosisi ya Meru Mkoani Arusha kwa ajili ya kuongoza harambee ya
kuchangia fedha kwa ajili ya ukarabati wa kanisa hilo,iliyofanyika leo
Mkoani humo.
****
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa
amesisitizia tena kuwa tatizo la ajira kwa vijana ni jambo la hatari kwa
usalama wa nchi,wakati alipokuwa katika harambee ya kuchangia ukarabati
wa kanisa la kilutheri usharika wa Akyeri Meru mkoani Arusha, Mh
lowassa ameonya kuwa suala hilo lisiposhughulikiwa haraka litasababisha
hali ya hatari.
''tunashuhudia
maandamano katika mataifa ya ulaya vijana wakidai hali bora ya maisha
pamoja na ajira.hali hiyo tusipoangalia inaweza kutokea hapa nchini
kwetu.
huko
nyuma niliwahi kusema kuwa makanisa, mashirika na watu binafsi wasaidie
juhudi za serikali kutatua suala hilo''alisema Lowassa.
Lowassa
ambaye katika harambee hiyo aliongozana na marafiki zake, ambapo yeye na
familia yake pamoja na marafiki zake wamechangia kiasi cha shilingi
millioni 33.2.
Zaidi ya shilingi millioni 160 zikiwa ni fedha tasilimu pamoja na ahadi zilipatikana katika harambee hiyo.
Kwa
upande wake askofu Akyoo wa jimbo la Meru alimsifu Lowassa kwa
uchapakazi wake popote alipokuwa.''Wakati ulipokuwa Waziri Mkuu
ukimsaidia rais tulishuhudia uwezo wako mkubwa katika kufuatilia
majukumu yako''alisema na kuongeza kuwa Lowassa ni mtu wa ibada
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (wa tatu
kushoto) akiongozana na Askofu wa Kanisha hilo la Lutherani usharika wa
Akyeri,Dayosisi ya Meru Mkoani Arusha,Askofu Akyoo.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipokea
ahadi ya mchango kutoka kwa mmoja wa wamini wakati wa harambee ya
kuchangia ujenzi wa Kanisa la Lutherani usharika wa Akyeri,Dayosisi ya
Meru Mkoani Arusha.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiondoka
kanisani hapo baada ya kumalizika kwa harambee ya kuchangia ujenzi wa
Kanisa la Lutherani usharika wa Akyeri,Dayosisi ya Meru Mkoani Arusha.
No comments:
Post a Comment