December 17, 2012

KOFFI OLOMIDE AIVURUGA ROCK CITY KATIKA TAMASHA LA TUSKER CARNIVAL

Koffi Olomide akiliongoza skwadi lake la madensa jukwaani,full kujiachia.
Pichani shoto ni msanii kutoka THT,Rachel akionesha umahiri wake wa kucheza lingala huku Koffi Olomide akidekshia kwa mbaali hivi,palikuwa hapatoshi watu wangu.
Mwimbaji nyota wa Koffi Olomide,Cindy nae akionesha umahiri wake wa kujimwaya mwaya jukwaa,huku mashabiki (hawapo pichani) wakipiga miluzi na mayowe.
Wadau nao wakijichukulia taswira zao kwa ajili ya kumbukumbu.
Wakazi wa Mwanza walipfika kwenye uwanja wa ccm-kirumba walijionea vilivyo kwamba Koffi Olomide na kundi lake zima la Quartie Latin bado ni moto wa kuotea mbali.
Burudani ikiendelea jukwaani.
Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya SBL,Ephraim Mafuru, Anitha Msangi Maurice Njowoka na Patrick Kisaka kutoka kampuni ya bia ya Serengeti wakiwa katika picha ya pamoa usiku huu ndani ya uwanja wa CCM-Kirumba.
Sehemu ya wakazi wa Mwanza wakifuatilia kwa makini burudani.
Lwaaaaa....!! 
Msanii mahiri kutoka THT,Rachael kama kawaida nyonga yake laiiini inayosisimua mashabiki wake kila awapo jukwaani,na ndivyo kwa wakazi wa Mwanza walivyobaki kupiga mayowe ya shangwe usiku huu ndani ya CCM-Kirumba.
Ilikuwa ni burudani mwanzo mwisho.
Madansa wa Koffi Olomide wakipanda jukwaani kwa staili ya kipekee kabisa tayari kuangusha bonge la burudani kwa washabiki na wapenzi wa kundi la Quartie Latin.
Cindu mwanamuziki mwenye sauti nyororo.laini na safi kabisa akiimba jukwaani kwa umahiri mkubwa huku akipambwa na madensa wa bendi hiyo ya Quartie Latin.
Cindy akiimba kwa hisia jukwaani.
Back up ya ukweli ya Koffi Olomide akiimba kwa pamoja jukwaani.
Mwanamuziki mahiri wa Koffi Olomide,Cindy akipewa maiki mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa CCM-Kirumba usiku huu tayari kwa kuzikonga nyoyo za mashabiki wa kundi lao.Onesho la Tusker Carnival limeandaliwa na kampuni ya Prime Time Promotioni ikishirikiana kampuni dada ya Clouds Media Group,likidhamiwa na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake cha Tusker Lager "bia bora,marafiki wa kweli".
Mwanamuziki Koffi Olomide sambamba na mwimbaji wake nyota Cindy wakiwasili usiku huu kwenye uwanja wa CCM-Kirumba tayari kwa kuwatumbuiza wakazi wa jiji la Mwanza.
Cindy akiwaza jambo jukwaani kwa utulivu mkubwa.





 

No comments:

Post a Comment