Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ambaye pia ni Mtafiti Mkuu Kiongozi, Dk. Leonard Mboera kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) akizungumza wakati wa Warsha ya siku mbili kati ya Waandishi wa Habari na Watafiti wanasayansi nchini Tanzania juu ya namna ya uandikaji taarifa za kiutafiti sambamba na namna watafiti wanavyotakiwa kuandaa taarifa zao za utafiti ili ziwafikie wananchi. Warsha hiyo ilifanyika Mo Makuu ya NIMR mwishoni mwa wiki.
Mtafiti Mwanasayansi Dk. N Range kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) akizungumza jambo wakati wa Warsha hiyo ya Siku mbili jijini Dar es Salaam mwisho mwa wiki iliyopita.
Washiriki mbalimbali ambao ni wtafiti wanasayansi pamoja na Wanahabari wakiwa katika Warsha hiyo.
Meneja Mahusiano wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Coletha Njelekela akizungumza wakati wa Warsha hiyo ya Siku mbili iliyowakutanisha Wanahabari na Wanasayansi Watafiti kutoka NIMR mwisho mwa Wiki Iliyopita.
Dawati la Uratibu w warsha hiyo baina ya Waandishi wa Habari na Wanasayansi watafiti kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) wakiwa kazini.
Baadhi ya Watafiti wakifuatilia kwa umakini mada zilizokuwa zikijadiliwa.
Mpigapicha Mwandamizi kutoka Shirika la Utangazaji la TBC, Abeid Butu akichangia mada katika warsha hiyo ya siku mbili iliyo wakutanisha wanahabari na Wanasayansi Watafiti.
Mwandishi Mwandamizi wa Gazeti la Mwananchi, Elias Msuya akichangia mada katika warsha hiyo. Pamoja na e ni Wanasayansi watafiti kutoka NIMR.
Mwandishi wa Habari wa Kujitegemea na mmoja wa waezeshaji katika Warsha ya Wanahabari na Watafiti wa NIMR, Rose Ruben akifafanua jambo.
Mtafiti Mwanasayansi, Sia
Malekiakutoka NIMR, akiwasilisha utafiti wake mbele ya Wanahabari na Watafiti wenzekake mbalimbali wakati wa Warsha hiyo. Utafiti huo ulihusu Upungufu wa Wahudumu wa Afya na Utoaji Huduma za VVU/UKIMWI Tanzania.
Mtafiti na Mkuu wa Idara ya Maadili ya watafiti, Basiliana Emidi akiwa na Meneja Uhusiano wa NIMR, Coletha Njelekela (kulia) wakati wa Warsha hiyo.
No comments:
Post a Comment