Baadhi
ya wafanyakazi wa Benki ya Azania wakiwa katika mchezo wa mpira wa
miguu wakati wa siku yao ya Michezo iliyofanyika mwishoni mwa wiki
katika ufukwe wa bahari katika Hoteli ya Jangwani Sea Breeze iliyopo
jijini Dar es Salaam
*****
BENKI ya
Azania ya Tanzania imesema kuwa michezo ni muhimili unaosaidia
kuimarisha afya, kuleta umoja na kukuza utendaji kazi wa watu katika
maeneo mbalimbali ikiwemo sekta ya kibenki. Hayo yalibainishwa na
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania, Bw. Charles Singili, wakati wa
hafla ya wafanyakazi wa benki hiyo ya mwaka 2012 iliyowakutanisha
wafanyakazi wa makao makuu na matawi yake yote yaliyopo Dar es salaam.
Wafanyakazi
hao walishiriki katika michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu,
mpira wa wavu, kuogelea pamoja na kucheza muziki, tukio lililofanyika
mwishoni mwa wiki katika ufukwe wa bahari katika hoteli ya Jangwani Sea
Breeze jijini Dar es Salaam. “Hili ni tukio muhimu sana kwetu kama
Benki ya Azania kwa kuwa tunahitaji wafanyakazi wetu kuwa katika afya
nzuri kimwili na kiakili na tunatambua kuwa kupitia michezo tutaendelea
kuwa na wafanyakazi wenye afya nzuri na wataweza kuongeza juhudi katika
utendaji kazi wao na kuleta umoja ndani yetu.
“Matukio
kama haya yanayokutanisha wafanyakazi wetu, yanatusaidia katika
kufahamiana vizuri, kubadilishana mawazo na kutafakari kwa umoja wetu
nini tufanye zaidi katika kuhudumia wateja na kukuza huduma zetu na
kuleta tija zaidi katika sekta ya kibenki,” alisema Bw. Singili.
Alisema
kuwa baada ya kufanyakazi mwaka mzima wakiwa wanahudumia wateja wao na
kuwasaidia kufikia malengo yao kwa kuwapatia huduma za kifedha na za
kibenki, benki hiyo iliona ni vyema kupata japo siku moja ya kushiriki
katika michezo na wakati huo huo kuweza kutafakari kwa pamoja ni jinsi
gani benki itaongeza tija katika kuwahudumia wateja pamoja na kuchangia
katika ukuaji wa uchumi wa nchi kwa ujumla.
“Benki ya
Azania haishiriki katika michezo tu lakini pia inasaidia makundi
mbalimbali ya kijamii katika mahitaji ya kiafya, kielimu na kutoa
misaada kwa mayatima na makundi mbalimbali ya wasiojiweza. Tunatoa
michango yetu tukitambua umuhimu wa makundi haya katika kusaidia kujenga
Taifa letu,” mkurugenzi huyo alisema.
Bw. Singili aliongeza kuwa benki hiyo hutoa misaada hiyo ikiwa ni kama
jukumu la benki katika kuirudishia jamii sehemu ya mapato yake wakati
benki inatengeneza faida.
No comments:
Post a Comment