Kikosi cha zamani cha Taifa Stars
Kikosi cha Kilimanjaro Stars kilichoriki Tusker Challenge Cup Uganda
Kikosi cha Zanzibar Heroes kilicho shika nafasi ya 3 Tusker Challenge Cup Uganda.
WAKATI
vikosi vya timu za Kilimanjaro Stars na Zanzibar Heroes vilivyokuwa vinashiriki michuano ya Kombe la Tusker
Cecafa Chalenji jijini Kampala, vinarejea Dar es Salaam na Zanzibar hii leo,
kesho Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania anataraji kutanga kiksi kipya cha
timu hiyo.
Kocha
Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen kesho Jumatatu saa sita mchana katika Ofisi za
Shirikisho la Soka nchini anataraji kutangaza kikosi hicho ambacho dhahiri
kitaundwa na Wachezaji wa timu mbili za taifa za Bara na Visiwani ambazo
zilishiriki michuano iliyomalizika jana jijini Uganda na kuonesha uwezo wao
mkubwa kisoka.
Kikosi
chake hicho kipya kitakachoingia kambini jioni ya Desemba 12, 2012 jijini Dar
es Salaam kujiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya mabingwa wa Afrika, Zambia
(Chipolopolo) itakayofanyika Desemba 22, 2012 katika Uwanja wa Taifa.
Jumapili
(Desemba 9, 2012). Timu hiyo itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere (JNIA) saa 11 kamili jioni kwa ndege ya Precision Air.
No comments:
Post a Comment