December 04, 2012

AIRTEL YAZINDUA PROMOSHENI MPYA KWAAJILI YA WATEJA WAKE MWISHO WA MWAKA 2012

 Meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa promosheni mpya ya Airtel "AMKA MILIONEA" kushoto ni Meneja Huduma za Ziada Airtel Francis Ndikumwami na Afisa matukio wa Airtel kulia,  kujiunga na promosheni hiyo mteja atatakiwa kutuma neno SHINDA au WIN kwenda namba 15595 bure na atapokea maswali atakayoyajibu na kukatwa sh 350 kila sms na kupata point
zitakazomuwezesha kushinda.

*********
Airtel yazindua promosheni mpya kwaajili ya  wateja wake mwisho wa mwaka 2012

* Airtel yazindua promosheni  "AMKA MILIONEA" kwa wateja wake.
* Kwa siku 90  wateja 875 wa Airtel kujizolea shilingi milion 401

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imezindua promosheni mpya ilikuweza kuwazawadia wateja wake wakati wa msimu huu wa mwisho wa mwaka.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo kwa waandishi wahabari  Meneja wa huduma za ziada wa Airtel Francis Ndikumwami alisemakwamba "Airtel  inakutoa fursa nyingine kwa Tanzania kushiriki na
kushinda zawadi ya fedha taslimu wakati wa msimu huu wa sherehe. 
 
Leotunazinduzi "AMKA MILIONEA" amabazo jumla ya zawadi za fedha taslimu zenye thamani ya shilingi milioni 401zitatolewa ndani ya siku 90 tu.
 
Kutakuwa na washindi wa kila siku, kila wiki, kila mwezi na zawadikubwa moja itatolewa mwisho wa promosheni, katika promosheni hiiwateja wa Airtel 875 watazawadia hizo milioni 401.

AMKA MILIONEA itakuwa na washindi wa aina tofauti tofauti . Washindiwa kila siku, kila wiki na kila mwezi, AMKA MILIONEA itahakikisha kilasiku kunawashindi 10 kushinda kila siku na watagawana jumla yashilingi  3,000.000, kila wiki jumla ya shilingi milioni 6,000,000 zitashindaniwa na washindi 10 na kila  mwisho wa mwezi  mshindi mmojaatashinda kitita cha shilingi milioni 30 wakati milioni  50, 0000Tshsitaenda kwa mshindi mmoja mwisho wa promosheni hii.

Akizungumza jinsi ya kujiunga na promosheni hiyo  Meneja Uhusiano waAirtel Jackson Mmbando alisema, Ili mteja aweze kushiriki inabidiatume neno WIN/SHINDA kwenda namba 15595 bure na utakuwa ujiungajiunga, Baada kujiunga mteja atakuwa atapata ujumbe kutoka 15656 na kupata maswali ambayo atajibu na akipata sahihi atapata ponti20 akikosea atapata ponti 10. Na kwakila ujumbe atakaotuma atatozwa kiasi cha shilingi 350 pamoja na kodi.

Amka milionea imeanza leo (jana) Desemba 3, 2012 itaenda hadi Machi 2, 2013 Vigezo Muhimu

Mshiriki mmoja hawezi kushinda zaidi ya 1 ya kwa zawad ya kila siku .Mshiriki mmoja hawezi kushinda zaidi ya 1 yakwa zawadi ya kila wikiMshiriki mmoja hawezi kushinda zaidi ya 1 zawadi ya kila mwezi.
 
Mshiriki mmoja unaweza kushinda mara moja zawadi ya kila siku, maramoja zawadi ya kila wiki  na mara 1 zawadi ya kila mwezi. Lakini pia
anaweza akajishindia zawadi kubwa ya mwisho wa promosheni
Kujiunga.

Tuma neno "WIN / Shinda", kwenda namba 15595 ( bure), na kisha utapokea ujumbe wa ukaribisho utakaombatana na maswali utakayojibu.
 
Kila jibu sahihi mteja atapata pointi/alama 20 na akikosea atapata pointi 10 zitakazomuwezesha kushinda, ukijibu maswali mengiunajionge zea nafasi ya ushindi.

No comments:

Post a Comment