December 04, 2012

SELCOM PAYPOINT SASA KUUZA VOCHA ZA ZUKU

Meneja wa matangazo na Masoko wa Kampuni ya SelCom wireless Paypoint Juma Mgori , akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutangaza rasmi Kampuni hiyo kuanza kuza vocha za kulipia King’amuzi cha Zuku kupitia vituo mbalimbali vya Selcom paypoint. Kushoto ni Meneja Mkuu wa Zuku Tanzania Fadhil Mwasyeba.
Meneja wa matangazo na Masoko wa Kampuni ya SelCom wireless Paypoint Juma Mgori , akifafanua jambo kwa wanahabari (hawapo pichani) juu ya huduma wanazotoa ikiwa ni pamoja na ulipiaji wa Bili mbalimbali kama za simu mitandao yote, Luku, Startime, Tiketi za Treni za jijini Dar es Salaam,kulipia ada za Mitihani NECTA, kuangalia matokeo na sasa Zuku.
Meneja Mkuu wa Zuku Tanzania Fadhil Mwasyeba  akizunguma na waandishi wa habari wakati wa makubaliano ya mkataba wa kujiunga na SelCom kwa ajili ya Malipo ya Zuku.
Meneja Mkuu wa Zuku Tanzania Fadhil Mwasyeba kushoto akizunguma na waandishi wa habari wakati wa makubaliano ya mkataba wa kujiunga na SelCom kwa ajili ya Malipo ya Zuku, wengine ni  Meneja wa matangazo na Masoko wa Kampuni ya SelCom wireless Paypoint Juma Mgori   na Meneja wa Bidhaa na uboreshwaji wa viwango Julio Batilia .
 Waandishi wa habari wakichukua nukuu ya mambo yanayozungumzwa.
Meneja Mkuu wa Zuku Tanzania Fadhil Mwasyeba (wapili kushoto) akibadilishana hati ya makubaliano ya kulipia king'amuzi cha Zuku kwa njia ya mtandao na Meneja wa matangazo na Masoko wa Kampuni ya SelCom wireless Paypoint Juma Mgori,  makubariano hayo yamefanyika Dar es salaam Leo kwa ajili ya kurahisisha hudumu hio. Wanaoshuhudia ni Maofisa kutoka Selcom na Zuku.

No comments:

Post a Comment