Mkurugenzi
Mkuu wa Airtel Tanzania Bw Sam Elanagaloor akielezea huduma ya 'One
network' kwa waandishi wa habari (hawapo pichani)ambapo leo airtel
imezidua huduma itakayowaweze wateja wa airtel wanaosafiri kwenda India,
Srilanka na Bangladesh kusafiri na laini zao za Airtel Tanzania na
watafaidi kupokea simu bila malipo yoyote na kufurahia kupiga simu kwa
viwango nafuu zaidi wakiwa katika shughuli zao za kusherehekea kumaliza
mwaka, biashara au matibabu (leo) katika ofisi kuu ya Airtel Tanzania
*******
Jumatano
12 Desemba 2012, Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel katika msimu huu
wa sikukuu imewawezesha wateja wote nchini kuendelea kutumia laini zao
za Airtel Tanzania wakiwa India na kufurahia kupokea simu bila makato
yeyote na kuwahakikishia uhuru wa kuongea wakati wa msimu huu wa
sikukuu.
Akitoa
ufafanuzi juu ya huduma hii ijulikanayo kama "One Network Asia"
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bw Sam Elanagaloor alisema" wateja wetu kutoka
Tanzania wanaosafiri kwenda India, Srilanka na Bangladesh wataweza
kusafiri na laini zao za Airtel Tanzania na watafaidi kupokea simu bila
malipo yoyote na kufurahia kupiga simu kwa viwango nafuu zaidi wakiwa
katika shughuli zao za kusherehekea kumaliza mwaka au biashara
"Tunafahamu
kuna watanzania wengi wanapata matibabu nchini India, kuna watanzania
wengi wanasoma nchini India, Tunaamini kwa kupitia huduma hii
tutawawezesha watanzania wengi wanaotembelea na wale wenye ndugu nchini
India kuwasiliana bila gharama yeyote sio tu katika kipindi hiki cha
msimu wa sikukuu ila na siku za usoni. Mteja anachotakiwa kufanya ni
kuongeza muda wa maongezi kwenye laini yake ya Airtel Tanzania na
kufurahia huduma za Airtel" aliongeza Elangalloor.
Mbali
na kuzinduliwa kwa huduma hii inayota unafuu kwa wateja wa Airtel
watakaofanya safari zao kwenda India Srilanka na Bangladesh, wateja wa
Airtel wote pia wataendelea kufurahia huduma huduma ya 'One network'
(kutumia laini zao za nyumbani) katika nchi 17 za Afrika ikiwemo:
Kenya, Uganda, Malawi, DRC, CongoB, Madagascar, Nigeria, Ghana, Rwanda,
Zambia, Niger, Gabon, Burkina, Sierra L,Chad, Tanzania.
"Hili ni la uhakika kabisa kwa kuwa mtandao wetu ni mpana, wateja wa
Airtel wanaposafiri kwenye nchi hizo wanaunganishwa na kupiga simu kwa
bei nafuu, kuongeza salio kwa kutumia vocha za nchi walizotoka wakiwa
popote, pamoja na kuunganishwa na huduma ya internet" alimaliza kwa
kusema Elangalloor.
No comments:
Post a Comment