A
Tukio hilo limetokea kijijini
hapo siku ya Alhamis tarehe 06/12/2012 majira ya saa sita usiku, ambapo Polisi
kupitia mkakati wake wa Polisi Jamii na Ulinzi Shirikishi walipata taarifa za kuuzwa
kiholela kwa Dawa mbalimbali za Binadamu katika kijiji hicho.
Uchunguzi wa awali ulianza mara moja kuhusiana na taarifa hizo,
ambapo taarifa zilizomuhusisha
mwenyekiti huyo kuhusika na biashara hiyo zilipatikana. “Wanakijiji katika eneo
hilo walikiri kwamba mwenyekiti huyo amekuwa akiuza Dawa hizo mara kwa mara.”
Mwenyekiti huyo amekuwa akifungua
chumba cha kuhifadhia Dawa katika Zahanati hiyo kisha kuiba na kwenda kuziuza
yeye akiwa na mshirika wake ambaye tumemkamata, amekuwa akifanya hivyo kwa kuwa
yeye ndiye mwenye Dhamana ya kutunza
funguo za chumba hicho.
Aidha mshirika wake
alipofanyiwa upekuzi nyumbani kwake alikutwa na makopo ya Dawa aina za
Paracetamol, Piritoni na nyingine za aina mbalimbali ambazo ni miongoni mwa
zilizoibwa katika zahanati hiyo, thamani ya Dawa hizo bado hazijafahamika hadi
sasa.
Upelelezi unakamilishwa ili
watuhumiwa hao wafikishwe mahakamani mara moja.
Natoa wito kwa wanajamii kwa
kupitia mkakati wa Polisi jamii na Ulinzi Shirikishi kuendelea kushirikiana na
Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa mbalimbali za wahalifu na uhalifu ili kwa
pamoja tuweze kuzuia na kupambana kero na matishio ya aina mbalimbali katika
maeneo yetu.
No comments:
Post a Comment