Mkurugenzi
mtendaji wa kampuni ya Zara Tours,Zainab Ansell akizungumza na
Wanahabari mapema leo mchana,Mikocheni jijini Dar kuhusiana na mafanikio
waliyoyapata tangu kuanzishwa kwa kampuni hiyo mnamo mwaka 1987 ikiwemo
kupata tuzo 2012 Humanitarian,mjini London,Uingereza.Aidha
Bi Zainab ameeleza kuwa kupata kwa tuzo hiyo ndani ya kampuni yake ni
heshima kubwa kwake pamoja na wadau mbalimbali wa mambo ya utali,aidha
ameongeza kuwa kampuni yake itajijengea heshima na kuongeza juhudi kubwa
katika suala zima la kuutangaza utalii wa ndani ya nchi hii.kulia ni
Meneja Mkuu wa kampuni ya Zara Tours,Leila Ansell.
Baadhi ya Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakimsikiliza Mkurugenzi
mtendaji wa kampuni ya Zara Tours,Zainab Ansell alipozungumza nao
mapema leo mchana kuhusiana na mambo mbalimbali ya kampuni yake na namna
gani ya kuutangaza utalii wa ndani na nje na namna ya kuisaidia jamii
katika nyanja mbalimbali.Kwa habari zaidi kuhusiana na Zara Tours bofya; www.zaratours.com.
No comments:
Post a Comment