November 23, 2012

RAIS WA ZANZIBAR AENDELEA NA ZIARA YAKE VIETNAM,

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiwa na ujumbe wake wakitoa heshima ya salamu baada ya kuweka shada la mauwa  katika kumbusho wa Baba wa Taifa la Vietnam, Ho Chi Minh Mousoleum,akiwa katika ziara rasmi ya Kiserikali,ya wikimoja nchini humo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiwa na ujumbe wake wakiongozwa kwa gwaride maalum wakati alipowasili  katika kumbusho wa Baba wa Taifa la Vietnam, Ho Chi Minh Mousoleum,kuweka shada la mauwa,akiwa katika ziara rasmi ya Kiserikali,ya wikimoja.[
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed shein, akiwatambulisha Viongozi aliofuatana nao kwa Makamo wa Rais wa  Vietnam Bibi,Nguyen Thi Doan,walipowasili Ikulu ya nchi hiyo kwa mazungumzo,ya  kuimarisha uhusiano na Ushirikiano baina ya pande zote, akiwa katika  ziara rasmi ya wiki moja  nchini humo.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed shein, akisalimiana na Mawaziri na Viongozi mbali mbali wa Nchini Vietnam ,alipofika ikulu ya nchi hiyo kwa mazungumzo na Makamo wa Rais  Vietnam Bibi, Nguyen Thi Doan, akiwa katika  ziara rasmi ya Kiserikali nchini humo ya wiki moja.

No comments:

Post a Comment