November 20, 2012

WAUAJI WA SWETU FUNDIKIRA WAHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA

Watuhumiwa wa kesi ya Mauaji ya Marehemu Swetu Fundikira,wakiwa Mahakamani mchana wa leo kabla ya kusomewa hukumu yao.
Askari wa JWTZ waliotiwa hatiani hii leo na Mahakama Kuu ya Tanzania kwa mauaji ya Swetu Fundikira, Koplo Ali Ngumbe(Kushoto) na Sajini Rhoda Robert. Watuhumiwa hawa na mwenzao mmoja Mohamed Rashid wamehukumiwa Kunyongwa hadi kufa.
 
Hayati Swetu Fundikira enzi za uhai wake.
******
ASKARI wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Sajent Rhoda Robert, Koplo Ally Ngumbe na Mohamed Rashidi waliokuwa wakikabiliwa na Kesi ya mauaji ya Marehemu Swetu Fundikira imetolewa leo na Askari hao kuhukumiwa Kunyongwa hadi kufa.

Hukumu hiyo iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa na ndugu jamaa na marafiki wa Swetu duniani kote ilitolewa leo katika Mahakama Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam.

Washtakiwa hao watatu wametiwa hatiani baada ya kufanya kosa hilo siku ya Jumamosi tarehe 23 Januari, 2010 kwa kumpiga bila huruma Swetu Fundikira katika maeneo ya Kinondoni katika makutano ya barabara  za Mwinjuma na Kawawa jijini Dar es salaam mpaka kusababisha kifo chake.

Baada ya kusomwa kwa hukumu hiyo vilio vimetawala kwa ndugu wa watuhumiwa hao huku baadhi ya watu wakidai sheria imechukua mkondo wake ipaswavyo.

1 comment:

  1. What do we learn out from it?....No one is above the law!.

    ReplyDelete