November 20, 2012

UJUMBE WA MABALOZI WA JUMUIYA YA ULAYA PAMOJA NA WAWAKILISHI WA WAFANYA BIASHARA WATEMBELEA MAMLAKA YA BANDARI TANZANIA (TPA) LEO

 Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison akiwaonyesha Mabalozi wa Jumuiya ya Ulaya,na baadhi ya wawakilishi wa wafanya Biashara, Muswada  wa Uboreshaji wa Maswala ya Usajili wa Meli uliowasilishwa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kama sehemu ya Kuboresha Sheria ya Usajili wa Meli Kisiwani  Humo. Mabalozi wa Jumuiya ya Ulaya wamefanya ziara kwenye Bandari ya Dar es Salaam ili kuona shughuli zinazofanywa na Mamlaka hiyo.
Mabalozi wa Jumuiya ya Ulaya pamoja na wawakilishi wa  Wafanya biashara wakiwa katika Jengo la Abiria la Kampuni ya Azam Marine kuangalia namna usalama wa abiria ulivyo kabla ya kupanda Meli za abiria kulekea Unguja. Mabalozi hao wamefanya Ziara Katika Bandari ya Dar es Salaam leo ili kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka ya Bandari Tanzania.
Meneja Uendeshaji wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Bw. Patrick Namahuta, akiwapa maelezo ya namna Bandari ya Dar es Salaam inavyofanya kazi Mabalozi wa Jumuiya ya Ulaya . Mabalozi hao wametembelea Bandari hiyo leo, kujionea mabadiliko yaliyofanywa na Mamlaka mwaka mmoja baada ya wao kutembelea Mamlaka hiyo Mwezi Oktoba 2011.
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe(Mwenye Suti Nyeusi) akipata maelezo ya namna mashine ya kukagulia Tiketi  maalum za Abiria wanaoingia kwenye Meli kuelekea Unguja kutoka kwa mmoja wa Maafisa wa Kampuni ya Azam Marine. Waziri wa Uchukuzi aliongozana na Mabalozi wa Jumuiya ya Ulaya na baadhi ya Wafanyabiashara(Hawapo Pichani), ili kujionea namna ambavyo Bandari ya Dar es Salaam inavyofanya kazi hasa kwenye swala la Usalama wa abiria .

No comments:

Post a Comment