MWIMBAJI maarufu wa
muziki wa Injili nchini, Rose Muhando na mwenzake Enock Jonas
(Zunguka) wanatarajiwa kutia chachandu katika tamasha la kwanza kubwa kufanyika
Mkoani Kagera.
Tamasha hilo la Shangwe Kagera
lina lengo la kuielimisha jamii na kuamsha mwamko wa kusaidia watoto yatima na
wanaoishi katika maisha magumu.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Beula
Communications Ltd, ambao ni waandaji wa tamasha hilo,Melkizedeck Mutta anasema
kuwa matayarisho ya tamasha hilo yanaendelea vizuri kutokana na mwitikio mkubwa
wa watu mbalimbali waliojitokeza kushiriki.
Pia, Mutta anasema bendi ya
muziki ya wazawa mkoa huo, Kakau Band pamoja na vikundi vingine vya
wanakwaya wa makanisa mbalimbali, kikundi cha watoto yatima
wanatarajia pia kutumbuiza.
Mutta anasema tamasha hilo la
aina yake linatajiwa kufanyika Uwanja wa Kaitaba na pia
kwenye ukumbi wa Lina’s mjini Bukoba, siku ya Uhuru, Desemba 9.
“Mpaka sasa tumekamilisha
sehemu kubwa ya matayarisho hayo ikiwamo kulipia uwanja pamoja
sehemu ya malipo kwa wasanii ambao watashiriki,” alisema.
Pia, mkurugenzi huyo aliwaomba
wadhamini zaidi na wadau wengine wa maendeleo na watoto kujitokeza kushiriki
ili kuwasaidia jamii hasa watoto yatima na wengine wanaoishi katika mazingira
magumu.
Lengo la Tamasha:
Ni kuhamasisha jamii kuishi
kwa amani,kupendana na kusaidia watu wengine hasa wasiojiweza kimaisha ili
na wao wajione ni sehemu yao.
Katika kutambua
hilo kampuni yetu iliamua kufanya utafiti mdogo nakugundua changamoto nyingi
katika Mkoa wa Kagera, mojawapo ni kuwa na watoto wengi wanaoishi
katika mazingira magumu. Baada ya kuliona hili, tulitembelea vituo mbalimbali
vya kulelea watoto hao, mojawapo ni Tumaini Children’s Centre kinachomilikiwa
na Kanisa la Kiinjili la Ki lutheri Tanzania (KKKT).
Kituo hiki kinalea watoto wote
bila kujali kabila,jinsia wala dini zao, kwa sasa kituo hiki
kinahudumia watoto zaidi ya 800, kwa kuwapatia elimu,chakula, malazi n.k ambapo
kwa muda mrefu kimekuwa kikipata msaada toka Sweden ambao kwa sasa wametangaza
kuusitisha kwa maelezo kuwa jamii ya Watanzania inapaswa kujifunza na kuanza
kuhudumia watu wao wenyewe.
Kutokana na hilo ndiyo maana
tumeonelea tuwe na tamasha la kuamasisha jamii ili ianze kuona umuhimu wa
kusaidia wenzao wanaohitaji msaada.
No comments:
Post a Comment