November 19, 2012

AIRTEL TANZANIA NA UNESCO WAZINDUA RADIO JAMII LOLIONDO MKOANI ARUSHA



Waziri wa Sayansi Mawasiliano na Technojia Prof. Makame Mbarawa akijaribu mtambo wa radio kwa kutangaza moja kwa moja (live) kupitia radio ya jamii LOLIONDO FM mara baada kumalizika kwa  hafla ya uzinduzi rasmi  wa radio hio ya jamii iliyowezeshwa kwa ushirikiano kati ya Airtel na shirika lisilola kiserikali UNESCO katika kijiji cha Ololosokwani kilichopo Loliondo Wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha. Waliomzunguka wawakilishi  Airtel na Unesco wakiwa na wenyeji wa kijiji cha Ololosokwani.
Waziri wa Sayansi Mawasiliano na Technojia Prof. Makame Mbarawa akifungua jiwe la msingi kuashiria uzinduzi rasmi wa radio ya jamii ya LOLIONDO FM wakati wa hafla maalum ya uzinduzi wa radio kijijini Ololosokwani. Uwekwaji wa redio hiyo  ya jamii umezeshwa kwa ushirikiano kati ya Airtel na shirika lisilo la kiserikali UNESCO katika kijiji cha Ololosokwani kilichopo Loliondo Wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha. Kulia ni mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Bi, Beatrice Singano na wakwanza shoto muwakilishi wa UNESCO bi Vibeke Jensen


Waziri wa Sayansi Mawasiliano na Technojia Prof. Makame Mbarawa akisalimiana wananchi wanakijiji wa kijiji cha Ololosokwani kilichopo Loliondo Wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha ambapo waziri huyo alikuwa mgeni rasmi wa katika ufunguzi  wa radio ya jamii pamoja na miradi mingine ilikiwemo ujenzi wa nyumba za kimasai za kisasa
Wadau wawezeshaji wa radio ya jamii ya LOLIONDO FM wakiwa wamepozi katika picha ya pamoja na waziri wa Sayansi Mawasiliano na TechnogiaProf. Makame Mbarawa mara baaada ya uzinduzi wa radio hiyo kijijini Ololoskwani Kiongozi


 ******
Maeneo zaidi ya 10 Tanzania bara na kisiwani kufikiwa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kishirikiana na shirika lisilo la kiserikali UNESCO kwa pamoja wamezindua Radio jamii katika kijiji cha Ololosokwani kilichopo Loliondo Wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha.

Uzinduzi huo ulihudhuriwa na kufanywa na Waziri wa mawasiliano sayansi na technologia Mh Makame Mbarawa.

Mradi wa Radio za jamii ni program maalum inayoendeshwa na Airtel kwa kushirikiana na UNESCO yenye lengo la kusaidia jamii zilizo na changamoto mbalimbali ikiwemo za mila potofu, elimu duni, ukeketwaji, imani za kishirikina, maendeleo duni , ukandamizaji wa wanawake na watoto na  hangamoto inginezo.

Maeneo hayo pia mbali ya kuwa na changamoto huduma za mawasiliano ni duni na upatikanaji wa huduma za radio kwaajili ya kuelimisha jamii ni changamoto kubwa.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa radio hiyo, Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Technologia Mh Makame barawa alisema” ninawapongeza Airtel na UNESCO kwa jitihada zenu hizi katika kuendeleza mawasiliano chini hasa vijijini, mimi nimefurahishwa sana kuona wadau hawa wanavyojiunga najamii ya kijijini hapa  a kuwaunganisha na sehemu nyingine za dunia kwa kuweka radio hii ya Loliondo FM ili kuwawezesha upata habari na taarifa muhimu kwa maendeleo ya taifa”.

Hii ni fulsa ya pekee kwenu wakazi wa kijiji cha ololosokwani pamoja na vijiji jirani kuinua shughuli zetu za kiuchumi, kutumia radio hii kutoa maoni na elimu, Naamini vipindi vitakavyorushwa vitakuwa
vimelenga jamii husika na kuwa chachu ya kuleta ufanisi mkubwa katika mabadiliko na maendeleo kwa ujumla”.

Aliongeza Mbarawa Akiongea kwa niaba ya Airtel Mkurungezi wa Mawasiliano Bi Beatrice
Singano Mallya alisema “Airtel inajisikia furaha kuwa nafasi ya kuchangia maendeleo jamii  nchini Tanzania, tunaamini kwamba kupitia redio hii na kwa kupitia mtandao wetu ulioenea zaidi wananchi wamaeneo haya na vijiji takribani 14 vya jirani watanufaika na kuwepo kwa redio Loliondo fm hapa  lolosokwani.

Tunategemea kuona maisha ya ndugu na jamaa zetu wa jamii ya wamasai na wageni waliopo hapa yakibadilika  kwa kasi katika Nyanja zote” “sasa Wakazi wa ololosokwani watapata nafasi kwa kupitia radio  hii, kutangaza utamaduni wao, kuboresha na kupata uongozi bora, kutangaza biashara zao na ukuza soko huku wakitumia huduma ya Airtel money kupata malipo na kuhifadhi pesa zao kwa usalama zaidi” alisema Singano Singano aliongeza kuwa “Mbali na Radio tumeweza pia kuwawezesha wakazi wa kijijini hapa kupata huduma ya internet kupitia Multimedia center tuliyoijenga na kuiwekea mtandao wetu wenye spidi wa 3.75G, Aliongeza Singano Naye mwakilishi kutoka UNESCO bw,  Ali-amin Yusuph lisema “UNESCO inayofuraha kuona mradi wa radio unakuwa na kuwafikia wananchi wengi nchini kwa shirikiano wa Airtel,  kuwepo kwa radio hii kutaunganisha wakazi wa Ololosokwani na wale wa maeneo mengine nchini na dunia kwa ujumla.

UNESCO tunayo miradi mingi sana ya kusaidia jamii na Mradi wa
Radio hapa Olosokwani umetusaidia kuona maeneo mengine mengi  ya kuweza kusaidia jamii hii ya kimasai, leo tunayo miradi mbalimbali tuliyoianzisha  hapa ikiwemo Mradi wa Solar (umeme wa jua) ambao utawawezesha akina  mama kupata kipato.

Kwa kupitia mradi huu wakazi wa hapa wamepata sehemu za kuchajia simu zao na kuweza kufanya shughuli zinazohitaji umeme kwa malipo kidogo”.

“Halikadhalika tumeweza kurekebisha nyumba za kimasai na kuzifanya ziwe na muundo wa kisasa unaotoa moshi nje ya nyumba na kuzifanya ziwe na kiwango bora” Alimaliza kwa kusema mwakilishi kutoka UNESCO bw, Ali-amin Uzinduzi wa kituo hicho cha radio ijulikanayo kama LOLIONDO FM
uliambatana na ugawaji wa vitabu  vya masomo ya sayansi kwa wanafunzi wa shule mbalimbali kijijini humo kutoka kwa kampuni ya Airtel  ikiwa ni kuwahamasisha wanafunzi wengi kupenda fani ya sayansi wakiwa  tangu wadogo kitu ambacho kitachangia kuongeza idadi ya wataalamu wa sayansi hapa nchini
Airtel kwa kushirikiana na UNESCO inaendelea na mradi  wa radio jamii unaotegemea kufikia maeneo mengi zaidi nchini ikiwemo Sengerema Mwanza,  Karagwe Kagera,  Chake Chake Pemba, Makunduchi Unguja ,Pangani Tanga,  Kyela Mbeya , na Kalama Shinyanga.

No comments:

Post a Comment