Mkuu wa Polisi wilaya ya Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP)
Gilles Muroto akifafanua jambo wakati wa mkutano wa Ulinzi shirikishi
uliofanyika katika shule ya Msingi Sokoni One iliyopo katika jiji la Arusha.
mkutano huo uliofanyika tarehe 12.11.2012 uliwajumuisha askari wa jeshi la
Polisi, viongozi wa kata ya Sokoni one na askari wa vikundi vya Ulinzi shirikishi.
Maofisa wa Jeshi la Polisi waliokaa kutoka kushoto ni Mkuu wa Polisi
wilaya ya Arusha (SSP) Gilles Muroto, Mkuu wa kitengo cha Polisi Jamii mkoa wa
Arusha (SP) Mary Lugola na Mkuu wa kituo cha Unga Limited (SSGT) Shaban
Shaban wote kwa pamoja wakimpongeza kwa kumpigia makofi afisa Mtendaji wa Kata
ya sokoni One Bw.Gustafu Milambo(Aliyesimama) kutokana na kazi nzuri
anayeifanya kwenye kata yake juu ya uanzishwaji wa vikundi imara vya polisi
Jamii.
Mkuu wa kitengo cha Polisi Jamii mkoa wa Arusha Mrakibu wa Polisi (SP)
Mary Lugola akitoa elimu ya Polisi Jamii kwa askari wa vikund vya
ulinzi shirikishi katika mkutano uliofanyika shule ya Msingi Sokoni One
iliyopo kata ya Sokoni One jijini Arusha juzi tarehe 12.11.2012
Baadhi ya kikundi cha polisi Jamii cha mtaa wa Kanisani katika kata ya
Sokoni One wakisikiliza kwa umakini elimu ya Ulinzi
shirikishi iliyokuwa inatolewa na Maofisa wa Jeshi la Polisi mkoani hapa.
Mkutano huo ulifanyika juzi tarehe 12.11.2012 katika shule ya Msingi
Sokoni One iliyopo jijini Arusha.
Picha na Mahmoud Ahmad
No comments:
Post a Comment