Mtoto wa marehemu Aidan Libenanga,
Ramadhan Libenanga wa kwanza kushoto akishirikiana na ndugu, jamaa na
marafiki wakiingiza jeneza katika kaburi wakati wa mazishi ya mwandishi
huyo wa habari aliyefariki dunia Nov 18 mwaka huu mkoani Morogoro.
Mzee Aidan Hassan Libenanga enzi za uhai wake.
Waandishi wa habari mkoa wa Morogoro na
mikoa ya jirani wakiwa na mishumaa wakiwasha kwa ajili ya kuweka katika
kaburi la mpendwa wao Mzee Aidan Libenanga baada ya shughuli za mazishi
kukamilika.
Mke wa marehemu, Aidan Libenanga,
Elizaberth Libenanga (katikati) akisindikizwa na rafiki zake kuweka
shada la maua katika kaburi la mume wake katika makaburi ya Kola.
Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini
Abdullaziz Abood akitoa heshima za mwisho kwa mwandishi Aidan Libenanga
wakati wa kuaga mwili huo nyumbani kwake kota za Sabasaba Kiwanja cha
Ndege shughuli iliyoanza majira ya saa 7 mchana.
Mwandishi wa IPP MEDIA mkoa wa Morogoro Devotha Minja naye akitoa heshima zake za mwisho.
Meya wa Manispaa ya Morogoro Amiri Nondo naye akitoa heshima hizo.
Ramadhan Libenanga na kaka yake aliyembeba mtoto wakiaga mwili wa baba yao.
Mratibu wa miradi wa chama cha waandishi
wa habari mkoa wa Morogoro (MOROPC) Thadei Hafigwa akiaga mwili wa
marehemu Aidan Libenanga muda mfupi kabla ya kuelekea katika makaburi ya
Kola kwa ajili ya mazishi ya mpendwa wetu. (Picha Zote kwa Hisani ya www.jumamtanda.blogspot.com).
Mkuu wa wilaya ya Mvomero mkoa wa
Morogoro Anthony Mtaka akitoa salamu za uongozi wa mkuu wa mkoa huo Joel
Bendera wakati wa ibada ya mazishi ya marehemu Aidan Libenanga nyumbani
kwake.
Ndugu wa karibu wa Mzee Aidan Libenanga wakiangua kilio mara baada ya kuaga mwili wa mpendwa wao.
Mmoja wa watoto wa Mzee Libenanga akiwa ameshikwa na ndugu kuelekea katika gari kwa ajili ya kwenda makaburini.
Ni huzuni na vilio kwa ndugu, jamaa na marafiki wakati wa kuaga mwili wa Mzee Libenanga.
No comments:
Post a Comment