November 21, 2012

MATAIFA YA AFRIKA YATAKIWA KUAINISHA SERA NA MIKAKATI YA MAENDELEO YA VIWANDA NA ILE YA UMOJA WA AFRIKA

Mgeni Rasmi Waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Dkt. Abdallah Kigoda akitoa hotuba katika Maadhimisho ya 23 ya Siku ya Viwanda Afrika yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo, ambapo amesema hakuna nchi hapa duniani ambayo imepata maendeleo ya kudumu kwa wananchi wake bila kuendeleza viwanda, kwa sababu viwanda vinatoa ajira na hivyo kupunguza umasikini wa kipato kwa wananchi wanaozalisha bidhaa viwandani.

Akifungua maadhimisho hayo Mh. Dkt. Kigoda amesema Tanzania tunaendelea kujijengea msingi bora wa kuendeleza viwanda vyetu ambapo jumla ya viwanda vyote nchini ikijumuisha na mitambo ya kufua umeme ni takriban 733.

Mapema Mh. Dkt. Kigoda pia alizindua rasmi Ripoti ya Hali ya Ushindani wa Sekta ya Viwanda Nchini 2012 ambayo pamoja na mambo mengine imetoa mapendekezo kwa maeneo yanayoonekana yanahitaji msukumo ili kuongeza kasi ya uendelezaji viwanda.

Maudhui ya Ripoti hiyo iliyoandaliwa na Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na UNIDO yanashabihiana kwa karibu sana na kauli mbiu ya ya mwaka huu.

Kauli mbiu ya ya mwaka huu ni “Kuongeza Kasi ya Maendeleo ya Viwanda kwa Ajili ya Kukuza Biashara Baina ya Nchi za Afrika”.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI) Bw. Felix Mosha akizungumza machache kumkaribisha mgeni rasmi pamoja na wageni waalikwa katika maadhimisho hayo.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Dkt. Alberic Kacou akizungumzia Siku ya Viwanda Afrika na kusema kuwa ilitengwa na Umoja wa Mataifa mwaka 1989 kwa madhumuni ya kuzitaka nchi za Afrika pamoja na Jumuiya ya Kimataifa kubaini na kutambua umuhimu wa viwanda na mchango wake katika maendeleo ya Bara la Afrika.

Amesema Siku ya Viwanda Afrika kwa mwaka huu inaangazia umuhimu ambao biashara baina ya mataifa ya Afrika inaweza kuchangia kupunguza umasikini, kuongeza akiba ya chakula na lishe na kuwezesha maendeleo endelevu.

Uchimu wa Afrika mpaka sasa kwa kiasi kikubwa umekuwa ukitegeme kilimo kama uti wa mgongo, lakini viwanda ndio njia pekee ya kuweza kufanya mabadiliko yatayowezesha kunyanyua uchumi wa mataifa ya Afrika.

Moja ya vigezo vikubwa vya kufanya mabadiliko ni madiliko hali ya mifumo kutoka kilimo kuelekea viwanda.

Mgeni Rasmi Mh. Dkt. Kigoda akikata utepe kuzindua rasmi Ripoti ya Hali ya Ushindani wa Sekta ya Viwanda Nchini 2012 iliyoandaliwa na Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na Shirika la Umoja la Maendeleo ya Viwanda UNIDO, akisaidiwa na Mwenyekiti wa CTI Bw. Felix Mosha, akishudiwa na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Dkt. Alberic Kacou.
Imezinduliwa rasmi..!!
Pichani ni baadhia ya wadau waliohudhuria maadhimisho ya Siku ya Viwanda Afrika wakiwemo mawaziri, waheshimiwa mabalozi, waheshimiwa wabunge, makatibu wa kuu wa wizara, wakuu wa mashirika na waheshimiwa washirika wa maendeleo.
 
   
 
Mgeni rasmi katika Maadhimisho ya 23 ya Siku ya Viwanda Afrika Mh. Dkt. Kigoda katika picha ya pamoja na mawaziri wa serikali, makatibu wakuu wa wizara, wakuu na viongozi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa, wakurugenzi na maafisa wa taasisi mbalimbali na wadu wengine mara baada ya kukamilika uzinduzi wa ripoti na hotuba japokuwa kongamano bado linaendelea katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment