November 22, 2012

MIAKA 45 YA NDEGE INSURANCE YAFANA SANA

Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima (TIRA), Israel Kamuzora akitoa hotuba yake katika hafla ya kutimiza miaka 45 ya tangu kuanzishwa kwa Kampuni ya Bima ya Ndege na Uzinduzi wa Nembo Mpya ya Kampuni hiyo,iliyofanyika usiku wa leo kwenye hoteli ya Serena,jijini Dar es Salaam 
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Ndege,Sebastian Ndege (kulia) akizungumza machache juu ya Kampuni yake hiyo kabla ya kugonganisha Glass na Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima (TIRA), Israel Kamuzora (kushoto) ikiwa ni ishara ya pongezi kwa Kampuni hiyo kuadhimisha Miaka 45 tangu kuanzishwa kwake.Hafla hii imefanyika usiku wa leo kwenye hoteli ya Serena,Jijini Dar es Salaam.
Keki ya Kuadhimisha Miaka 45 ya Kampuni ya Bima ya Ndege (Ndege Insurance) ikikatwa.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Ndege (Ndege Insurance),Sebastian Ndege (kulia) akimuonyesha Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima (TIRA), Israel Kamuzora (pili kulia) nembo mpya ya Kampuni hiyo wakati wa uzinduzi wake rasmi ulioenda sambamba na kuadhimishwa kwa Miaka 45 ya tangu kuanzishwa kwa Kampuni hiyo.
Mfanyakazi aliekaa kwa kipindi kirefu kwenye Kampuni ya Bima ya Ndege,Bi. Eutropia Benedict akikabidhiwa tuzo na Mkurugenzi wa Kampuni hiyo,Justin Ndege.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Ndege,Sebastian Ndege (kushoto) akimkabidhi Tuzo ya heshima Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima (TIRA), Israel Kamuzora (kulia) kwa mchango mkubwa alioutoa kwenye Kampuni hiyo.
 
Wadau Mbalimbali walihudhulia hafla hiyo.
Mh. Mudhihir Mudhihir pia alikuwa ni mmoja wa Wageni waalikwa kwenye Hafla hiyo.
Waziri wa Zamani wa Mambo ya Ndani,Mh. Laurance Masha akiteta jambo na Mdau wakati wa hafla hiyo.
Wadau,toka kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa Benki ya NMB,Iman Kajura,Mbunge wa Kigamboni,Mh. Faustin Ndugulile pamoja na Mdau Haki Ngowi.
 
 
 
 
 
Wadau wakiwakilisha ndani ya hafla hiyo ya kuadhimisha miaka 45 tangu kuanzishwa kwa Kampuni ya Bima ya Ndege,iliyofanyika usiku wa leo kwenye hoteli ya Serena,Jijini Dar es Salaam.
Burudani kutoka SKYLIGHT Band ikitolewa,

No comments:

Post a Comment