November 22, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MAADHIMISHO YA SIKU YA TAKWIMU AFRIKA, DSM LEO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wananchi wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika, yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo Nov 22, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mkurugenzi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Brandina Chuwa, wakati alipokuwa akiwasili kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo Nov 22, 2012 kwa ajili ya kufungua rasmi Maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Ofisi ya Takwimu waliokuwa Meza Kuu, baada ya kufungua rasmi Maadhimisho hayo leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu waliohudhuria ufunguzi wa maadhimisho hayo baada ya ufunguzi rasmi uliofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Kamishna wa Sensa , Hajjat Amina Mrisho Said, wakati akiondoka katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo Nov 22, 2012 baada ya kufungua rasmi Maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika.

No comments:

Post a Comment