Mbunge wa
Jimbo la Babati Vijijini,Mhe. Jitu Vrajlal Soni (wa tatu kulia)
akizungumza wakati wa Harambee ya kuchangia Ujenzi wa Kanisa la Kiinjili
la Kilutheli Tanzania (KKKT) usharika wa Babati,Mkoani Manyara
leo.Wengine pichani toka Kushoto ni Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa
Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye
Harambee hiyo),Mbunge wa Babati Mjini, Kisyeri Chambiri na Kulia ni
Diwani wa kata ya Endamilay (CCM) Gesso Bajuta.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa
akimpongeza Mbunge wa Viti maalum Mkoani Manyara (Chadema),Mh. Pauline
Gekul mara baada ya kuchangia kwenye Harambee ya Ujenzi wa Kanisa la
Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) usharika wa Babati,Mkoani Manyara
leo.Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini,Mhe. Jitu Vrajlal Soni.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiendelea
kupokea michango mbali mbali kwenye Harambee ya Ujenzi wa Kanisa la
Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) usharika wa Babati,Mkoani Manyara
leo.
Baadhi ya
Waumini wa Kanisa hilo wakiwa kwenye Harambee hiyo ya Ujenzi wa
Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) usharika wa
Babati,Mkoani Manyara leo.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akihutubia
waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) usharika wa
Babati wakati wa Harambee ya kuchangia Ujenzi wa Kanisa hilo Usharika wa
Babati,Mkoani Manyara leo.
********
Na mwandishi wetu
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh
Edward Lowassa amesema wakati umefika sasa hapa nchini elimu ya
sekondari iwe ni elimu inayotolewa bure na kumwondolea mwananchi mzigo .
Lowassa
amesema hayo leo mjini Babati wakati wa harambee ya ujenzi wa Kanisa la
Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) usharika wa Babati.
Alisema
kwa sasa kila kata hapa nchini ina shule ya sekondari na huo ulikuwa
mpango wake akiwa Waziri Mkuu na alisimamia kikamilifu suala hilo na
kufanikiwa kwa asilimia mia moja.Shule hizo za kata ni maarufu kama
shule za Lowassa.
Hata hivyo kiwango kinachotolewa na shule hizo ni cha chini sana.
Waziri
Mkuu huyo mstaafu ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Monduli alisema sasa
wakati umefika kwa kila mtanzania kulizungumzia suala hilo bila ya woga
hususani wadau wa elimu na kuongeza kuwa.
''Ni
lazima tukubali na tujadili suala hilo kwa manufaa ya nchi kwa kila
mtanzania kukubali ushauri huo wa elimu ya sekondari kuwa ya
bure''alisisitiza na kuongeza kuwa kuwa ni vyema baada ya kulijadili
suala hilo la elimu ya bure ya sekondari tena elimu iliyo bora liwemo
kwenye ajenda za Chama cha Mapinduzi (CCM) za uchaguzi mkuu wa 2015.
Lowassa
alisema kuwa hivi karibuni Rais Jakaya Kikwete alitoa wito kwa shule za
sekondari kujenga maabara kwa wingi,hivyo kwa hiyo amesema ni suala
linalopaswa kuungwa mkono na kila mtanzania na pia elimu ya bure katika
sekondari nayo inapswa kuungwa mkono.
‘’Nasema
sasa wakati umefika elimu ya sekondari kuwa kama elimu ya msingi kwa
watoto kusoma bure kuanzia kidato cha kwanza hadi kidato cha nne
‘’alisema.
Lowassa
aliwaasa pia wadau mbalimbali hapa nchini kuwa mstari wa mbele kuchangia
elimu ili nchi hapo baadae iwe na vijana wenye elimu ya kutosha na ya
hali ya juu.
No comments:
Post a Comment