Rais wa Malawi, Bingu wa Mutharika amefariki hii leo Aprili 5,2011 baada ya kuugua ghafla ugonjwa wa Kukamatwa moyo "cardiac arrest" na kupelekwa kupata matibabu katika Hospitali ya Kamuzu mjini Lilongwe.
Habari ambazo zimeanza kusambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii nchini Malawi zinasemna kuwa madaktari katika Hospitali hiyo licha ya jitihada zao za kunusuru maisha ya Rais Mutharika lakibni ziligonga mwamba.
Mutharika (78) alipelekwa hospitali katika mji mkuu wa Lilongwe Alhamisi asubuhi baada ya kuripotiwa kuanguka.
"Rais amefariki dunia," alisema Afisa wa juu wa serikali ambaye hakutaka kutajwa jina lake.
Hospitalini hapo Mutharika alikuwa akiuguzwa na mkewe, Callista na mtoto wake wa tatu. Pia alikuwapo kaka, Petro Mutharika na Mkuu wa Utumishi katika serikali yake, Edward Sawerengera.
Waziri wa Afya Jean Kalirani na Mkuu wa Polisi, Petro Mukhito walikuwa pia huko.
Habari ya kifo cha Mutharika imeanza kuleta minong’ono kuhusu mustakabali wa siasa nchini Malawi ingawa Katiba inasema Makamu wa Rais ataongoza nchi hadi utakapofanyika uchaguzi ujao 2014.
Habari ya kifo cha Mutharika imeanza kuleta minong’ono kuhusu mustakabali wa siasa nchini Malawi ingawa Katiba inasema Makamu wa Rais ataongoza nchi hadi utakapofanyika uchaguzi ujao 2014.
Bingu wa Mutharika aliingia madarakani katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2004 na aliwahi kuwa ofisa wa Ngazi za juu wa Benki ya dunia na kushiriki vyema katika kuitetea nchi masikini Kusini mwa Afrika.
No comments:
Post a Comment