April 05, 2012

SABODO AKIPA CHADEMA MILIONI 100 KWA USHINDI WA ARUMERU MASHARIKI

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willbrod Slaa (kulia), akimshukuru mfanyabiashara maarufu nchini, Mustafa Sabodo baada ya chama hicho kupatiwa msaada wa sh. mil. 100, kwa kufurahishwa na ushindi wa Chadema katika uchaguzi uliofanyika  Jimbo la Arumeru Mashariki, Arusha Jumapili. Hafla hiyo ilifanyika, Dar es Salaam.
 Mfanyabiashara maarufu nchini, Mustafa Sabodo (kushoto) akitia saini kwenye hundi yenye thamani ya sh. mil. 100 alizotoa msaada kwa Chadema, baada ya kufurahishwa na ushindi wa chama hicho katika Jimbo la Arumeru Mashariki Jumapili. Kulia ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa chama hicho, Antony Komu. Hafla hiyo imefanyika leo nyumbani kwa Sabodo Upanga, Dar es Salaam.

Source:  Kamanda Mwaikenda

No comments:

Post a Comment