April 06, 2012

MATUKIO YA CHADEMA ARUSHA KATIKA PICHA

 Mahakama Kuu Kanda ya Arusha jana ilimvua Ubunge Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema baada ya hukumu ya Kesi ya kupinga matokeo iliyofunguliwa na wanachama wa CCM, mkoani humo Mwaka 2010 baada ya Uchaguzi. Picha mbalimbali zikionesha matukio mbalimbali ya jana baada ya hukumu hiyo. Picha ya Juu ni Wafuasi wa Chadema arusha wakilia kwa uchungu.
wanachama wa CCM ambao walifungua kesi ya kupinga matokeo na kupelekea Lema kuvuliwa Ubunge wakiwa Mahakamani kabla ya kunza kwa kusomwa hukumu hiyo.
 Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ambaye pia ni Mwekiti wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai (kushoto) akiwa katika kutafakari jambo. Kulia ni Godbless Lema.
 Lema akikumbatiana na Mbowe katika hali ya kufarijiana nje ya Ofisi za Chadema Arusha.
 Godbless Lema aliyekuwa Mbunge wa Arusha mjini kwa Tiketi ya Chadema akizungumza na jamaa zake kwa simu baada ya Hukumu hiyo jana.
 Godbless Lema akihutubia kusanyiko la wafuasi wa chama hicho jana nje ya ofisi za Chadema mkoa wa Arusha waliotaka kujua hatma ya chama.
  Godbless Lema akihutubia kusanyiko la wafuasi wa chama hicho jana nje ya ofisi za Chadema mkoa wa Arusha waliotaka kujua hatma ya chama.Kulia ni Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe.
 Ni simanzi kwa wana Arusha kuenguliwa kwa Kipenzi chao.
 Rwakatare akizungumza nje ya ofisi za CHADEMA
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe nae akihutubia wafuasui hao. Kulia ni Gobless Lema.

No comments:

Post a Comment