April 03, 2012

MKUTANO WA WADAU WA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA MKUU WA MKOA WA TABORA ASEMA WANANCHI WAELIMISHWE


 Mkuu wa mkoa wa Tabora Fatma Mwasa akizungumza na wadau wa mfuko wa bima wa afya NHIF mkoani Tabora.
 Mkuu wa mkoa wa Tabora Fatma Mwasa akiwa na Viongozi mbalimbali wa mfuko wa bima ya afya NHIF kwenye meza kuu.
Wadau mbalimbali wa mfuko wa bima wa afya wakiwa katika mkutano huo mkoani Tabora
 
 
 
Mkuu wa mkoa wa Tabora Bi.Fatma Mwassa amezitaka halmashauri za wilaya mkoani humo kuongeza juhudi katika kuihamasisha jamii kujiunga na mfuko wa Afya ya jamii ikiwa ni  hatua muhimu ya kuwawezesha kupata huduma ya matibabu kupitia mfuko huo.

Akizungumza katika mkutano wa wadau wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya uliofanyika mjini Tabora,mkuu huyo alisema halmashauri na wadau wengine wa mfuko huo  wanaowajibu katika kuuelimisha umma kuhusu mfuko huo ikiwa ni hatua muhimu  ya kufanikisha dhamira ya Serikali  kwa kila mtanzania kuwa kwenye utaratibu wa Bima ya Afya.

Alisema ni ukweli usiopingika kuwa gharama za matibabu zimekuwa zikipanda mara kwa mara huku akibainisha kuwa njia pekee ya kumkomboa mtanzania ni kumpa uhakika wa kutibiwa yeye pamoja na familia yake kupitia mfumo wa Mfuko wa Afya ya jamii ambao unaratibiwa na NHIF.
Pamoja na kuainisha masuala kadhaa ya faida za mFuko huo Mkuu huyo wa mkoa alitoa mfano kwa nchi nyingi duniani zimekuwa zikifanikiwa katika masuala ya Afya kupitia Mifuko ya aina hiyo.

“Kwa wenzetu suala la Bima ya Afya ni la lazima kwa kila mtu,hata kwa wengine wanaopata fursa ya kwenda nje ya nchi kusoma ni lazima uwe umejiunga vinginevyo hutaweza kupokelewa”alisema Bi.Fatma Mwassa

Hata hivyo kwa upande mwingine mkuu huyo alionesha masikitiko yake juu ya uchangiaji mdogo wa huduma ya  Mfuko wa Afya ya Jamii  CHF huku akianisha takwimu zinazoanzia Januari 2012,ambapo kati ya kaya 410,148 zilizopo mkoani Tabora ni kaya 14,860 tu ndizo zilizojiunga na mfuko huo ambayo ni sawa na asilimia 3.6.

Aidha pamoja na kuwa mkoa wa Tabora ndio chimbuko la la Mfuko huo wa Afya ya Jamii CHF ambao ulianzia wilayani Igunga kwa halmashauri zote hapa nchini lakini jambo la kushangaza bado halmashauri nyingine zilizopo mkoani Tabora zinashindwa kufanya vizuri katika kufikia lengo lililowekwa na Serikali.

Kwaupande mwingine mkuu huyo wa mkoa Bi.Fatma alilazimika kuwataka wadau na halmashauri kwa ujumla kutumia vikundi vya ushirika pamoja na vyama vya msingi kama njia muhimu itakayosaidia kuandikisha wananchi waliowengi kujiunga na CHF.

Mkutano huo wa wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ulihudhuria na baadhi ya viongozi wa ngazi ya juu kitaifa wa NHIF,Katibu tawala mkoa wa Tabora,Wakuu wa wilaya zote za mkoa wa Tabora,waheshimiwa wabunge,Viongozi wa halmashauri za wilaya na manispaa wakiwemo

No comments:

Post a Comment