April 03, 2012

Twanga Pepeta, Mashauzi Classic kupamba utambulisho wa Miss Tabata 2012 Pasaka

Bendi za African Stars “Twanga Pepeta” na Mashauzi Classic “Wakali wa Kujiachia” watatumbuiiza kwenye onyesho la utambulisho wa Miss Tabata 2012 siku ya Pasata katika ukumbi wa Dar Wes Park, Tabata.

Mratibu wa shindano hilo Godfrey Kalinga alisema jana kuwa bendi hizo mbili zitafanya maonyesho yao kabla ya warembo kutambulishwa na hata baada ya utambulisho zitaendelea kutoa burudani kali hadi majogo huku wapenzi wao wakisherekea sikuku ya Pasaka.

Kalinga alisema onyesho hilo maalum imeandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts chini ya udhamini wa Konyagi.

Pia alisema itakuwa ni onyesho maalum ya kusherekea sikukuu ya Pasaka na kutambulisha warembo watakaoshiriki kwenye shindano la kumsaka Miss Tabata 2012 ambalo limepangwa kufanyika mwezi ujao.

“Wapenzi wa muziki na urembo siku hiyo watapata fursa ya kuwaona warembo hao kabla ya kushiriki kwenye shindano la Miss Tabata ambalo limepangwa kufanyika mwishoni mwa Mei,” alisema Kalinga.

Mratibu huyo alisema warembo wanaotaka kushiriki kwenye shindano la Miss Tabata wanaendelea na mazoezi katika ukumbi wa Dar West Park, Tabata chini ya wakufunzi watatu - Beatrice Joseph, Neema Chaki na Bokilo Junior. 

Warembo hao ni  Neema Saleh (18), Paulina Valentine (18), Khadija Nurdin  (19), Phillos Lemi (20) na Mercy Mlay (21).

Wengine ni  Neema Innocent (19), Ellen Sule (22),  Wikllihemina Mvungi (20), Queen Issa (20), Suzane Deodatus (19), Everline Andrew (21), Josephine Peter (20) na Jamila Omary (19).  

Warembo hao wako zaidi ya warembo 10 kutoka Tabata watafuzu kushiriki kwenye shindano la kanda ya Ilala,  Miss Ilala baadaye mwaka huu.
Mrembo anayeshikilia taji la Tabata ni  Faiza Ally.

Warembo wa Tabata wamekuwa wakifanya vizuri katika mashindano ya Miss Tanzania ambapo mwaka juzi Consolata Lukosi alishinda nafasi ya tatu kabla ya kutangazwa kuwa balozi wa kinywaji cha Redds.

Katika shindano la mwaka juzi Julliet William pia alishinda nafasi ya tatu katika ngazi hiyo ya taifa.

No comments:

Post a Comment