Meneja Mawasiliano na Mtaalam wa habari za Mtandao, Matina G. Nkurlu akimvisha pete ya Uchumba Rachel Sindbar katika tafrija fupi iliyofanyika nyumbani kwa biharusi leo Mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro. Rachel ni mwanafunzi wa chuo Kikuu cha Dodoma na ni Miss UDOM 2010. Wawili hao wanataraji kufunga ndoa yao takatifu baade mwaka huu.
Tukiteta jambo na mshenga wangu kabla ya kumvisha pete ya uchumba mpenzi wangu Rachel..anaefatilia kwa umakiiini pembeni yangu ni mdogo wangu Mama Simon
Nikilishwa Cake ya kimila na mchumba wangu ikiwa ni ishara ya kukubalika katika familia yam zee Sindbard
Rachel alionesha kwa mbaaaaaaali kitu chake alichovishwa
Kutoka kushoto:Mjombake Rachel, Dadangu mkubwa DIA, Matina ,mchumbangu Rachel,Mdogo wangu Rehema,Mama mkwe, mdogo wake Rachel na Paul.
Hapo nimeingiza mkono mfukoni naichomoa pete huku mamangu kushoto aliekaa akiangalia nini kitatokea!Rachel atakuibali pete ya mwanae ya uchumbaaaa?
Wazee wakazi hao ndiyo waliofanikisha kila kitu na mambo ya Matina yakaenda Supa huko uchagani. maana kutoka Singida hadi Moshi si mchezo.
Hili ni pozi la Uchumba tu tungoje la siku ya ndoa jamani.
Blogu hii inawatakia kila la heri katika safari yao waliyoianza ya kuelekea katika ndoa na Mungu awabariki sana.
No comments:
Post a Comment