April 08, 2012

"Jacky Daniel" ndio iliyomuua Kanumba; UCHUNGUZI.

RPC wa Kinondoni-Charles Kenyela
POMBE kali (Whisky) aina ya Jacky Daniel, imetajwa kama chanzo cha kifo cha mwigizaji nyota wa filamu nchini, Steven Charles Kanumba aliyefariki usiku wa kuamkia jana nyumbani kwake, Sinza, Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Kinondoni, ACP Charles Kenyela amesema leo kwamba uchunguzi wa awali unaonyesha hivyo, lakini bado wanaendelea na uchunguzi zaidi, ili kujua zaidi.
ACP Kenyela amesema kwamba Kanumba wamefanikiwa kumuhoji mtuhumiwa wa kwanza katika tukio hilo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na katika maelelezo yake amekanusha kumsukuma Kanumba.
Vyombo vingi vya habari vilimnukuu ndugu wa Kanumba, Sethi jana akisema kwamba Lulu alimsukuma mwigizaji mwenzake huyo katika ugomvi wao wa wivu wa kimapenzi hadi akaanguka na kufariki dunia.
Akizungumza kutokana na maelezo ya Lulu, Kamanda huyo alisema kwamba; ugomvi wao ulitokana na Kanumba kutaka kumdhibiti Lulu wakati akizungumza na simu.
“Kanumba aliamua kumfuata Lulu nje huku akifoka kwa sauti, akitaka aelezwe kwa nini alitoka nje kupokea simu, huku akimtuhumu kuwa huenda alikuwa akizungumza na mwanaume mwingine.
Baada ya Lulu kuona Kanumba anamfuata, aliamua kukimbia kutoka nje ya geti, lakini kabla hajafanikiwa kufungua geti, Kanumba  alimkamata na kumrudishwa ndani. Kanumba akiwa amemshikilia, waliingia wote chumbani na kufunga mlango. Sasa haijulikani nani aliyefunga mlango, ingawa maelezo ya Lulu, anadai kuwa aliyefunga mlango ni Kanumba,”alisema Kamanda huyo. 
Akiendelea kumnukuu Lulu, Kamanda huyo anasema; “Baada ya Kanumba kufunga mlango, alimuona akilegea na kujigonga kisogo chake kwenye ukuta wa chumba hicho kabla ya kuanguka chini,”alisema.
Alisema uchunguzi wa tukio zima ukikamilika, hatua inayofuata ni kumpeleka Lulu mahakamani kama mtuhumiwa wa mauaji.

6 comments:

  1. nasema hivi hii ni moja ya ushahidi wa utendaji mbovu wa jeshi la polisi la nchi hii,kutowa habari za kichunguzi kabla haujakamilika kiasi cha kuhatarisha ushadidi kuingiliwa kutoka pande zote mbili mlalamikiwa na mlalamikaji ...WAKE UPP OUR POLICE OFFICERS,

    ReplyDelete
  2. sijawah kuona polisi wanaofanya upelelezi wa kijinga na wakutokuwa makini kama hawa wa Tz ni nini maana ya uchunguzi? unatupa taarifa huku unasemauchunguzi unaendeelea?

    ReplyDelete
  3. JAMANI POLISI WANAHARAKA GANI KUTOA TAARIFA HIZI KWANINI WASISUBILI RIPOTI YA DAKTARI KWANZA! AMA KWELI HII NI TANZANIA HAKUNA SEHEMU YOYOTE ILE DUNIANI, KWANI UKIKUTA POMBE NDANI NDO KANYWA YEYE MAREHEMU AU LULU AU MTU MWINGINE, IKIWA HAKUNA ALIYEKUNYWA POMBE SIKU HIYO UTASEMAJE?

    ReplyDelete
  4. acheni ubabaishaji nyie wachangaiaji wa juu hakuna kesi isiyokuwa na taarifa ya awali, hii inasaidia vigazeti vya udaku kuacha kuandika hovyo hovyo kwa nia ya kuuza magazeti,

    ReplyDelete
  5. Nathani hao police hawana ujuzi na hawakuusomea mwili wa binadamu.lulu ndio chanzo kukubwa halafu sasa hivi anatowa maelezo ya uwongo.wasichana hatari sana sana akiwa ni mdogo.huwa wana uongo wa hali ya juu sana.

    ReplyDelete
  6. Nafikiri elimu ya POLICE wetu bado ni ndogo sana kiupelelezi mbona wanajigonga sana.Hatakama wanawakomoa waandishi wa magazeti wasiandike taarifa za uongo,kwani polisi hawawezi kuwatia hatiani? Mi naona tunapotezeana muda kuongelea mambo haya kila siku badala ya kufanya mambo ya maendeleo,hili ndo tatizo letu wabongo,kitu kidogo tunachukua muda mrefu kudiscuss wakati nchi ni masikini.Vip tukianza mada nyingine ya maendeleo,KANUMBA KAFAFA JAMANI!!!!!!

    ReplyDelete