Rais jakaya Kikwete na Makamu wake Dkt Mohammed Gharib Bilal, wakiongozana katika Uwanja vya Ikulu Ndogo Bagamoyo wakati walipofika kuhudhuria sherehe ya ndoa ya mdogo wake na Rais Kikwete, Yusuph Kikwete, iliyofungwa leo mchana katika uwanja huo na kuhudhuriwa na watu mbalimbali pamoja na wake za viongozi.Bwana harusi, Yusuph Kikwete akiongozana na wapambe wake wakati wakiingia katika uwanja huo kwa ajili ya kufunga ndoa.Rais Jakaya, akifurahia jambo na Mama Zakhia Bilal (kushoto) na Mam Asha Bilal (wapili kulia).Rais Jakaya Kikwete na Makamu wake Dkt. Bilala, wakiwa katika meza kuu kwenye Sherehe hiyo iliyofanyika Bagamoyo leo.Bwana Harusi, Yusuph, akifungishwa ndoa na Sheikh. Bwana Harusi Yusuph na waumini wa dini ya Kiislamu wakiomba dua baada ya tendo la kufungishwa ndoa.Bwana Harusi, Yusuph Kikwete akiwa na mkewe Mariam Ombaka, baada ya kufungishwa ndoa. Mama Salma Kikwete (kushoto) akiwa na Mama Zakhia Bilal (katikati) na Mama Asha Bilal, wakati wakiwa katika sherehe hiyo ya ndoa ya mdogo wake na Rais Jakaya Kikwete, Yusuph Kikwete leo mjini Bagamoyo.Bwana harusi akipiga picha ya kumbukumbu ya pamoja na wake za viongozi.Miraji Kikwete, naye hakuwa mbali katika kunasa matukio, hapa alikuwa akimpiga picha baba yake mdogo.Rais jakaya Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na mkewe Mama Salma Kikwete na Bwana na Bi Harusi.
July 15, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)




0 comments:
Post a Comment