Jumuiya ya wanamitandao ya jamii (Social Networks) nchini inachukua nafasi hii kumpongeza Mwanahabari mwenzetu Jackson Mmbando (pichani kushoto akigawa misaada siku yake ya kwanza kazini Julai 18,2011) kwa kupata nafasi ya kupiga mzigo Airtel Tanzania kama bosi wa Mahusiano wa Kampuni hiyo ya simu za mikononi.
Jumjuiya inakutakia kazi njema na endeleza mahusiano yako mazuri na vyombo vyote vya habari ambavyo umekuwa ukifanya navyo kazi kwa ufanisi toka huko ulikotoka, na ambako pengo lako halitozibika kirahisi. Waswahili walinena, myonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Kaka kazi unaiweza!
Kila la kheri wewe na familia yako mpya ya Airtel
Jumuiya ya wanamitandao

No comments:
Post a Comment