July 18, 2011

Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini ya gonga Mwamba Bungeni

Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja (kati) Katibu Mkuu,David  Jairo (shoto) na Naibu Waziri Malima Kigoma Ali
HATIMAYE Bunge la Tanzania limeitilia ngumu Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2011/12 iliyowasilishwa Bungeni hapo Ijumaa iliyopita. 

Kufuatia hatua hiyo, Bunge limeritdhia kuahirishwa kwa wiki tatu baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ambaye ni Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni kuwasilisha ombi hilo Bungeni. 

Aidha Mbunge wa Kilindi, Beatrice Shelukindo (CCM), akichangia mjadala wa bajeti hiyo aliwasilisha barua Bungeni inayodaiwa kuwa iliandikwa na Katibu Mkuu wa Wizara, David Jairo, ikizitaka idara na taasisi zote za wizara hiyo zichangie Sh milioni 50 kila moja, kwa ajili ya kukamilisha maandalizi ya uwasilishaji wa makadirio hayo.

Msumari wa pili juu ya tuhuma hizo ulipigwa na  Mbunge wa Simanjiro, Christopher ole Sendeka (CCM) aliyetaka kujua mantiki ya fedha hizo takribani Sh bilioni moja na wakataka wizara ifafanue zimekusanywa kwa ajili gani. 

Fedha hizo zilitakiwa ziwekwe Geological Survey of Tanzania (GST) kwenye akaunti Namba 5051000068 NMB tawi la Dodoma. Baada ya kutuma fedha hizo, wizara ipewe taarifa kupitia ofisi ya DP kwa uratibu.

No comments:

Post a Comment