
Mwenyekiti wa CUF, Prof Ibrahim Lipumba kipunga kwa wafuasi na wanachama wa CUf leo wakati wa maandamano hayo ya Kudai Tume Huru ya Uchaguzi. Kulia ni Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad na kushoto ni Kaimu katibu Mkuu Zanzibar, Juma Haji Duni " Mjela jela".

Baadhi ya mabango ambayo yalikuwa na jumbe tata kutoka kwa wafuasi wa chama cha wananchi CUF.

Kikosi cha wana Ngangari cha Blue Guard kikiwa kimejipanga tayari kwa maandamano.

Maandamano yakizunguka Msimbazi katika kipita kushoto.

Palipotokea kuto kuelewana walitaka kushikana mashati wenye kwa wenyewe. Kufuatia kwa baadhi ya wafuasi kutaka kwenda kwa Msajili huku wengine wakitaka Kidongo Chekundu.

FFU wakiwapiga chabo wana CUF na kuwasubiria walianzishe.

Kojozi likisubiri amri lianze kujikoloea maji ya kuwasha.

Jamaa walijipanga kila idara...

Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba akimsikiliza Msajili wa Vyama vya Siasa nchini John Tendwa aliyepokea maandamano yao katika Uwanja wa Kidongo Chekundu.
Mroki naona kwa unazi na ukada wa CCM ulokujaa unafikia hatua mpaka unavunja maadili ya uandishi wa habari, unaripoti habari na wewe unakuwa sehemu ya habari, eti "FFU wakiwapiga chabo wana CUF na kuwasubiria walianzishe.." Kwa chuki zako zidi ya wapinzani unaona Cuf ni watu wavurugu tu (wakulianzisha), hivi ingekuwa ni maandamo ya ccm ungeandika hivyo??? Kwanini usiwe na maoni chanya tu, kwamba hao askari wanalinda usalama wa wandamanaji, badala yake umewafanya kama wameenda hapo kupambana wakati huo mkutano una baaraka zote za hicho chombo cha dola (jeshi la polisi)! Jifunze kuwa mwana demokrasia!
ReplyDeleteNautiakasi...sidhani kama unajua maadili ya uandishi, maana "Chabo" ni kuangalia tu hivyo haina tatizo. kwani jana mlikuwa hamjui mnatakiwa muende wapi. Kwanza amewapa Spread hapo CUF mnatakiwa mumshukuru sana Kidevu.
ReplyDeleteOya mdau, acha mchezmsho wewe jana mimi nimeshuhudia CUF mnapenda fujo eti mtu anasema wazi yupo radhi kufa kisa Chama mngekuwa mpo radhi kufa kwaajili ya imani za dini zenu zinavyotaka nchi isingekuwa na dhambi. Ona hao askari wake wabadilisheni mavazi hata pasi hawapiki hayo makoti na usikute yanachawa. Chadema oyeeeeeeeeeeeeeeeee.
ReplyDeleteTatizo la CUF kuna Wanachama, Mashabiki na Wafuasi, wanachama wachache wanamoyo na nia njema na chama klakini wapo wafuasi na mashabiki ambao wao huleta vurugu kila kukicha, ona hapo wenyewe kwa wenyewe walikuwa wanataka kukamatana mashati.
ReplyDeleteNimefurahishwa sana na picha ya saba...kojozi likisubiri amri lianze kujikoloea maji ya kuwasha. Nafikiri ulikuwa na nia ya kuandika Kojozi...lianze kujikojolea...na sio kujikoloea.
ReplyDeleteNawasilisha