August 20, 2008

Rukia Bruno afariki Dunia

MNENGUAJI maarufu wa Bendi ya FM Academia, Rukia Bruno (Pichani) amefariki leo mchana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam .Taarifa ya kifo zilipatakana kwa vyombo vya habari mbalimbali kupitia kwa mtu aliyejitambulisha kama kaka wa Mwanamuziki Nyoshi el Saadat ambaye mkewe amefariki.Katika mazungumzo ya simu alisema shemeji yake alikuwa Muhimbili ambako alilazwa kabla ya kujifungua mtoto aliyefariki wiki moja iliyopita na kuzikwa hospitalini hapo.“Habari za msiba za Bruno ni kweli na upo Sinza nyumbani kwa Nyoshi ambako familia ya marehemu ipo katika kikao cha kupanga siku ya maziko ya marehemu yatakayofanyika siku yoyote kuanzia sasa,” alisema Credo.Aidha, Bruno alisema hafahamu chanzo umauti wa Rukia ambaye ameacha mume na mtoto mmoja wa kiume anayeitwa Staloni.Kabla ya kuwa bendi ya FM Academia mnenguaji huyo alikuwa katika bendi ya Twanga Pepeta, Bendi ya Tamutamu ambazo alijipatia umaarufu mkubwa kutokana na uwezo wake wa kuwapa burudani mashabiki.

No comments:

Post a Comment