August 11, 2008

BASATA yaibana ZAIN


BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) kupitia kamati ya vibali imewapa muda wa siku nne Kampuni ya simu ya mkononi ya Zain kujieleza kutokana na kudaiwa kuingiza nchini kundi la Umoja Group toka Afrika Kusini bila kibali cha Baraza.

Kwa mujibu wa barua iliyoandikwa kwenda kwenye kampuni hiyo kutoka kwa Kaimu Katibu Mkuu wa baraza hilo D.Lauwo ilisema Kamati ya Vibali vya Wasanii imebaini kuwa kampuni ya Zain ilileta kikundi cha Umoja Group toka afrika Kusini bila kibali cha baraza.

Alisema kikundi hicho kilifanya onyesho katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam kwa ajili ya uzinduzi wa Kampuni hiyo bila kibali cha Kamati ya Taifa ya Vibali vya wasanii ambayo ndiyo yenye dhamana ya kutoa vibali vya wasanii wanaoingia nchini

Lauwo alisema kutokana na hali hiyo Kamati ya Vibali inaipa nafasi ya kutoa maelezo kwa maandishi kwa nini Kampuni hiyo isichukuliwe hatua za kisheria kwa uvunjaji huo wa makusudi kwa kuipa muda hadi Agosti 14,mwaka huu kuwa imepeleka maelezo katika baraza hilo.

Alisema kampuni ya Zain ilifanya hivyo wakati ikijua haina mamlaka wala haijasajiliwa kuingiza nchini vikundi vya sanaa na kufanya maonyesho huku mila,desturi na sanaa za nchi ya Afrika Kusini na Tanzania zinatofautiana na kampuni hiyo kwa makusudi ikaleta kikundi kilichocheza jukwaani wakiwa maungo ya miili yao nje.
Alisisitiza kuwa pia kampuni hiyo bila kufuata taratibu za uingizaji vikundi nchini,ilikusudia kuinyima serikali mapato yake halali kutokana na maonyesho yao na na kulenga kuwadhalilisha watanzania walioona aonyesho hayo na wasanii hao kwa kuvaa nusu uchi.

3 comments:

  1. BASATA waache ufala huo wasiwaonee wivu.
    Vikundi vya ndani tu vinawashinda kuvidhibiti wasivae nusu uchi.
    Wasela tuliburudika kishenzy.
    Wasilete hizo!

    ReplyDelete
  2. kumbe nikimleta msanii kuja kuimba kwenye bafudei yangu inabidi nilipe basata?Mapato ya serekali yameliwa na mafisadi ambao mnakwepa kuwakamata halafu wanadai hela ndogondogo.Basata wanameshindwa kutetea hatimiliki na mengineyo kwamaslahi ya wasanii wabongo na wanaweza kutoa tathmini tangu wanamuziki kutoka nje wameanzakuja hayo mapato wameyatumiaje na taifa au wasanii wa bongo wamefaidika na nini?
    Ni nani asiye jua utamaduni wa kiafrika kusini ulivyo?. Nilihudhuria tamasha moja Diamond Jubilee miaka ya 80 lilialikwa kundi kutoka hukohuko nikiwa bado mdogo na walivaahivyo hivyo.
    Wanenguaji wetu je hawachukuliwi hatua yoyote serious kila siku wanakuja na mbinu mpya Basata get real organise your selves and make a concrete Baraza kwamanufaaya wasanii wetu

    ReplyDelete
  3. sijafagilia kabisa hiyo staili wanayocheza hapo wameiga kabisa hiyo na ya kundi la umoja lipo south africa.watanzania acheni kuiga iga muwe wabunifu.

    ReplyDelete