July 28, 2008

Warembo katika Michezo

Baadhi washiriki wa shindano la VodaCom MissTanzania,2008 wakicheza mpira wa Wavu katika ufukwe wa South Beach Hotel, ulioko Mjimwema Kigamboni, Dar es Salaam kuadhimisha siku maalum ya michezo. Shindano hilo linatarajiwa kufanyika Agosti 2 mwaka huu kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam.
Baadhi washiriki wa shindano la Vodacom miss Tanzania 2008 wakichuana vikali katika mchezo wa mpira wa Wavu katika ufukwe wa South Beach Hotel, ulioko mjimwema kigamboni Dar es Salaam, kuadhimisha siku yao ya michezo kabla ya shindano hilo linalotarajiwa kufanyika Agosti 2 mwaka huu kwenye viwanja vya Leaders jijini humo.Miss 3: Washiriki wa Vodacom Miss Tanzania 2008, wakimhoji mtoto Josephine aliyetoka kuokota kuni huko Mjimwema Kigamboni Dar es salaam juzi, wakati walimbwende hao walipokwenda kuadhimisha siku maalum ya michezo kwenye ufukwe wa South Beach Hotel, Mji Mwema, Kigamboni, Dar es Salaam juzi.
Mmoja wa Baadhi washiriki wa shindano la Vodacom miss Tanzania 2008,Nadya Ahmedi akipanda ngamia ikiwa ni sehemu za shamrashamra kuadhimisha siku yao ya michezo kwenye ufukwe wa South Beach Hotel, Mjimwema, Kigamboni jijini Dar es Salaam juzi.

No comments:

Post a Comment