ASKARI WA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA -JWTZ KIKOSI CHA LUGALO ANADAIWA KUMUUA KWA RISASI MKEWE USIKU WA KUAMKIA LEO.
HABARI TOKA NDANI YA KIKOSI HICHO ZINAMTAJA ASKARI HUYO KWA JILA LA ZUNGU AMBAYE ALIKUWA ANAFANYA KAZI KATIKA CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI HOSPITALI YA LUGALO.
IMEFAAHAMIKA KUWA CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI UGOVI WA KIMAPENZI ULIOTOKANA NA ASKARI HUYO KUFUMANIA SMS ZA MAPENZI KATIKA SIMU YA MKEWE SIKU KADHAA ZILIZOPITA NA ALIMFUKUZA MKEWE HUYO NA KWENDA NYUMBANI KWAO NDANI YA KIKOSI HICHO.
JUMATATU USIKU ALIMUITA AKIWA LINDONI KATIKA GETI DOGO LA KUINGILIA HOSPITALINI HAPO NA KUMSHAMBULIA KWA RISASI TANO NA KUSABABISHA KIFO CHAKE.
ASKARI HUYO ANADAIWA BAADA YA KUMALIZA KAZI HIYO ALIAGIZA MAJI YA KUNYWA NA KUSHUSHIA KABLA YA KUSALIMISHA SILAHA KWA WENZAKE AMBAO WALITAKA KUTIMUA MBIO ALIPOKUWA AKIWAFUATA.
HIVI SASA ZUNGU ANASHIKILIWA NA POLISI JIJINI DAR ES SALAAM KWA MAHOJIANO ZAIDI.
No comments:
Post a Comment