Nafasi Ya Matangazo

June 10, 2024

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele, akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Tume na Viongozi wa Dini uliofanyika leo tarehe 10 Juni, 2024 mkoani Dar es Salaam.  
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima, R. K akiwasilisha mada kwenye mkutano wa Tume na Viongozi wa Dini. 
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele, akiendesha majadiliano wakati wa mkutano wa Tume na Viongozi wa Dini uliofanyika leo tarehe 10 Juni, 2024 mkoani Dar es Salaam.  
Baadhi ya viongozi wa dini waliohudhuria mkutano huo wakifuatilia mada. 

Baadhi ya viongozi wa dini waliohudhuria mkutano huo wakifuatilia mada. 
Baadhi ya viongozi wa dini waliohudhuria mkutano huo wakifuatilia mada. 


Mada ya uboreshaji ikifanyika kwa vitendo.
*************
Na. Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imekamilisha maandalizi muhimu kwa ajili ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ikiwa ni pamoja na ununuzi wa vifaa vya uandikishaji vinavyojumuisha BVR Kits 6,000.

Hayo yamebainishwa leo tarehe 10 Juni, 2024 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima, R. K wakati akiwasilisha mada kwenye mkutano wa Tume na Viongozi wa Dini. 

Mkutano huo umefanyika sambamba na mkutano wa Tume na Taasisi na Asasi za kiraia ikiwa ni muendelezo wa utaratibu wa Tume wa kuwashirikisha wadau wa uchaguzi kabla ya kuanza rasmi kwa uboreshaji wa Daftari. 

Bw. Kailima amesema BVR Kits hizo zitatumia vishkwambi kuchukua taarifa za wapiga kura ikiwemo picha, saini na alama za vidole. 

“BVR Kits za sasa zinatumia mfumo endeshi wa android na uzito wake ni kilogramu 18, awali zilikuwa zinatumia mfumo endeshi wa window na uzito wa kilogramu 35, amesema Bw. Kailima. 

Amesema Mfumo wa Uandikishaji wa Wapiga Kura (Voters Registration System-VRS) umefanyiwa usanifu na kuboreshwa ili kukidhi aina ya BVR Kits za sasa ambazo zinatumia programu endeshi ya android.

Wakati akifungua mkutano huo, Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele amesema, BRV Kits hizo zitakuwa rahisi kubeba na kufanya zoezi la uboreshaji wa Daftari kuwa rahisi haswa kwenye maeneo ya vijijini ambapo watendaji hulazimika kubeba vifaa kwa umbali mrefu.

Amesema mfumo wa teknolojia hii ya BVR hutumika katika kumtambua mtu na kumtofautisha na mwingine.  Uandikishaji huu wa wapiga kura utahusisha uchukuaji wa alama za vidole vya mikono, picha na saini na kuhifadhiwa kwenye kanzidata ya wapiga kura, amesema.

Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura utazinduliwa mkoani Kigoma tarehe 01 Julai, 2024 na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (MB).
Posted by MROKI On Monday, June 10, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo