Nafasi Ya Matangazo

April 12, 2024

Mwakilishi wa Familia ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Edward Sokoine, Balozi Joseph Sokoine akimtazama Rais Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu wakati wa kumbukizi ya miaka 40 ya baba yao.
Na Ahmed Sagaff - MAELEZO
Mfumo wa maji uliopo katika vijiji vya Wilaya ya Monduli mkoani Arusha ni wa miaka ya 1970 wakati vijiji hivyo vikiwa na watu wachache hivyo upatikanaji wa maji haukidhi mahitaji.

Mwakilishi wa Familia ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Edward Sokoine, Balozi Joseph Sokoine ameyasema hayo leo mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan katika maadhimisho ya miaka 40 ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Hayati Edward Sokoine.

"Tunashukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutusaidia kutatua changamoto ya maji safi na salama kwani tuna imani kuwa mradi wa maji unaotoka Arusha kuja kwetu kijijini Monduli utamaliza uhaba wa maji," Balozi Sokoine amemweleza Rais Samia.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amearifu kuwa Rais Samia amekusudia kujenga barabara ya lami yenye urefu wa kilomita 11.66 kutoka Ngareshi hadi Monduli Juu ambapo Hayati Sokoine amezaliwa.

Pamoja na hilo, Rais Samia amesema watu wengi hawamjui Hayati Edward Sokoine hivyo Serikali itamuenzi kwa kufanya kazi kwa weledi.

“Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, asilimia 81 ya Watanzania wako chini ya umri wa miaka 40. Hii ina maana kwamba kati ya Watanzania watano, ni mmoja tu ndiyo alikuwa amezaliwa kabla ya Edward Sokoine hajafariki dunia mwaka 1984," amearifu Rais Samia.

Rais Samia amesema Watanzania wanne kati ya watano hawana kumbukumbu zao wenyewe wala hawakuishi kuona uongozi wa Sokoine.
Posted by MROKI On Friday, April 12, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo