Nafasi Ya Matangazo

April 14, 2024

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na waliokuwa walinzi wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Hayati Edward Moringe Sokoine wakati wa Kumbukumbu ya miaka 40 tangu kifo chake, iliyofanyika Monduli mkoani Arusha tarehe 12 Aprili, 2024.

Kulia ni aliyekuwa Mlinzi Mkuu Abihudi Michael Luila aliyekuwa gari ya nyuma wakati ajali inatokea na kushoto Mlinzi wa zamu Yusto Chuma ambaye alikuwa gari moja na Hayati Sokoine. Chuma wakati huo naye alijeruhiwa vibaya sana na kulazwa chumba cha wagonjwa mahututi kwa siku 14.

Hayati Sokoine alifariki dunia tarehe 12 Aprili, 1984 kwenye ajali ya gari iliyotokea Wami Dakawa Wilayani Mvomero mkoani Morogoro.
Posted by MROKI On Sunday, April 14, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo