Nafasi Ya Matangazo

March 29, 2024

 




Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bw.Kaspar Mmuya ameendelea na ziara yake ya kikazi ya ukaguzi wa miradi na kuongea na watumishi kwa lengo la kujitambulisha Katika Halmashauri za Mkoa wa Dodoma ambapo Leo Machi 28, 2024 ametembelea Halmashauri ya Wilaya ya Dodoma Mjini.

Kufuatia uzinduzi wa kampeni ya "Kero yako wajibu wangu", Bw.Mmuya ameendelea kuwa sisitiza watumishi kuwa na wajibu wa kusikilza na kutatua kero za wananchi kwa nafasi zao. Hayo ameyasema katika Kikao chake na watumishi wa Halmashauri hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa Umonga Jijini Dodoma.

“Ni vyema kujua vipaumbele na  wajibu wako wa Kusikiliza Kero za wananchi wanaotuzunguka tukiwa wawakilishi wao na uongozi mliopewa una jukumu la kutatua kero za wananchi katika Mitaa yetu na dhana ya kuwajibika inaenda Sabamba na utaratibu na kuipa ubora kazi yako.

“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anawajibika ipasavyo kwa kuleta fedha za miradi katika jamii na kama Msimamizi wa hizo fedha unapaswa kuzingatia ubora wa majengo yanayojengwa na kama kiongozi wajibu wako ni kuhakikisha hizo fedha zinatumika vizuri kama ilivyoelekezwa na usiwe chanzo cha kuwa kero kwa wengine" Amesema Bw. Mmuya.

Vilevile, ametilia mkazo suala la kuongeza ufaulu mashuleni, kuondoa utoro kwa wanafunzi, upandaji na utunzaji miti, mahusiano bora mahala pa kazi, uwajibikaji katika kila ngazi aliyonayo mtu.

Aidha, Katibu Tawala Mkoa amekagua mradi wa ujenzi wa Madarasa 08 na matundu 10 ya vyoo kwa ajili ya wanafunzi wa Kidato cha tano katika shule ya Sekondari Mtumba iliyopo kwenye kata ya Mtumba ambayo ilipokea fedha kiasi cha shilingi Milioni 201.

Mradi mwingine ni ujenzi wa vyumba 08 vya madarasa na matundu 10 ya choo katika shule ya Sekondari Zulu iliyopokea kiasi cha shilingi Milioni 201 na ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya iliyopokea shilingi Bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa Maabara, jengo la wagonjwa wa nje ( OPD), jengo la mama na mtoto, Jengo la Mionzi, Jengo la Dawa, jengo la kuhifadhia maiti na kichomea taka.
Posted by MROKI On Friday, March 29, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo