Nafasi Ya Matangazo

March 27, 2024







Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde ameanza ujenzi wa viwanja vya michezo ya mpira wa kikapu(_basketball_),mpira wa pete(_netball_) na mpira wa wavu(_volleyball_) katika eneo la shule ya Sekondar Kiwanja cha Ndege Jijini Dodoma.

Ujenzi huu unatokana na ahadi ambayo Mbunge Mavunde aliitoa wakati wa mahafali ya wanafunzi wa kidato cha IV  alipokuwa Mgeni Rasmi.

Akizungumza na wanafunzi leo asubuhi alipiwatembelea shuleni,Mbunge Mavunde amesema kiwanja hicho ambacho kitatumika kwa matumizi ya aina tatu ya michezo kitakuwa ni cha kisasa na kitasaidia kukuza michezo na vipaji vya wanafunzi wa Dodoma Jiji.

Pamoja na ujenzi huo,Mbunge Mavunde ameahidi kuweka taa katika uwanja huo ili uwe unatumika muda wote,kugawa seti za michezo na kununua tanki la kuhifadhi maji.

Akitoa taarifa ya maendeleo ya shule,Mkuu wa Shule Sekondari Kiwanja cha Ndege Ndg. Daniel. ameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mh Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ujenzi wa madarasa na fedha Tsh 50,000,000 za umaliziaji ujenzi wa maabara na kuongeza pia kukamilika kwa ujenzi wa michezo hapo shuleni utasaidia kuimarisha afya za wanafunzi na kukuza vipaji vyao kupitia michezo.

Akitoa shukrani zake,Diwani wa Kata ya Kiwanja cha Ndege  Mh. Amos Mbalanga amemshukuru Mbunge Mavunde kwa ujenzi wa miundombinu ya viwanja vya kuimarisha michezo na kuahidi kusimamia ujenzi wake kukamilika kwa wakati.
Posted by MROKI On Wednesday, March 27, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo