Nafasi Ya Matangazo

March 16, 2024








Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii  leo  tarehe 16 Machi, 2024 imetembelea Mradi wa PSSF wa Jengo la Kitega Uchumi la Rock City Mwanza na kuelekeza taarifa ya mradi huo iandaliwe upya na kuwasilishwa mbele ya Kamati baada ya taarifa iliyowasilishwa kutojitosheleza.

Awali Kamati hiyo iliwasili eneo la Rock City ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Mhe. Fatma Hassan Toufiq na kupokelewa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe.  Patrobas  Katambi,  Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhandisi Cyprian  Luhemeja na Watendaji wa PSSF wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu, Bw. Abdul-Rzaq Badru.

 Aidha mara baada ya kupokelewa  Wajumbe wa Kamati hiyo walitembezwa katika maeneo mbalimbali ya Jengo la Rock City kabla ya kukaa kikao cha kupokea taarifa ya utendaji kazi ya mradi huo.

Hata hivyo baada ya taarifa hiyo kuwasilishwa Wajumbe wa Kamati walionesha kutoridhiswa na jinsi taarifa ilivyoandaliwa ikiwemo kukosa maelezo ya kina.

Kufuatia hali  hiyo na baada ya Wajumbe wa Kamati kujadiliana Mwenyekiti wa  Kamati,  Mhe. Fatma Toufiq alisema  taarifa hiyo inapaswa iandaliwe na iwasilishwe upya mbele ya Kamati.

Kufuatia maelekezo hayo, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe.  Patrobas  Katambi alisema wamepokea maelekezo ya Kamati na watafanyia kazi.

Kamati ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii ipo katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo tangia tarehe 12 Machi, 2024 na  imeshafanya ukaguzi wa miradi katika Mikoa ya Tabora na Mara na tangu jana Ijumaa tarehe 15 Machi, 204 ipo Mkoani  Mwanza kwa ajili ya kazi hiyo.
Posted by MROKI On Saturday, March 16, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo