Wananchi wakiwa wamefurika katika Banda la Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Naliendele kujifunza teknolojia mbalimbali za kilimo kwenye Maonyesho ya Nanenane 2023 yanayofikia tamati leo Agosti 8, 2023 viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
******************
Na Dotto Mwaibale, Lindi
WANANCHI kutoka Mikoa ya Lindi, Mtwara na
Ruvuma wakiwa wamefurika katika Banda la Taasisi ya Utafiti kwa Kilimo Tanzania
(TARI) Naliendele mkoani Mtwara kwenye Maonyesho ya Nanenane 2023 Kanda ya
Kusini yanayofanyika Viwanja vya Ngongo mkoani Lindi kujionea na kujifunza
teknolojia mbalimbali za kilimo.
Katika Maonesho hayo watafiti wa kilimo wa TARI
wanaonesha na kutoa elimu za teknolojia za kilimo za kuvutia jambo
lililosababisha banda hilo kufurika wakulima na wananchi kwa lengo la
kujifunza.
Akizungumza na waandishi wa habari katika banda hilo kwa niaba ya
Mkurugenzi wa Kituo hicho Dk. Fortunus Kapinga kuhusu maonesho hayo Mtafiti wa
Kilimo Bakari Kidunda ambaye pia ni Mratibu wa Uhalishaji Teknolojia na
Mahusiano alitaja baadhi ya teknolojia ambazo zinaoneshwa na kutolewa kwa wakulima ni za mazao ya korosho, ufuta, karanga, mihogo, viazi vitamu, kunde, choroko, mbaazi, mahindi
na uwele.
Kidunda alitumia nafasi hiyo kuwaeleza wakulima kuwa katika kituo chao cha Naliendele wamekuwa hawana msimu bali wameweka teknolojia
ambazo zinaonekana kwa mwaka mzima kwa ajili ya wakulima kujifunza hatua
mbalimbali za ukuaji wa zao husika kuanzia likiwa kwenye kitalu, shambani, utumiaji wa viatilifu, udhibiti wa
magonjwa na uvunaji wake.
Mkulima
Mathayo Milanzi kutoka Wilaya ya Nanyumbu alisena amevutiwa na teknolojia
zinazofundishwa na TARI na kuwa moja ya teknolojia hizo ni kilimo cha ndizi
aina ya Mtwike ambapo awali alipokuwa akilima kwa kutumia kilimo cha mazoea
alikuwa akipata mazao kiduchu.
"Zamani ndizi nilizokuwa nikivuna nilikuwa
nikizibeba kichwani lakini baada ya kupata mafunzo ya kilimo cha kisasa
nimekuwa nikivuna ndizi nyingi hadi nalazimika kukodi pikipiki kwa ajili ya
kuzisafirisha kwenda kwenye soko," alisema Milanzi.
Milanzi alisema TARI wamekuwa mkombozi kwa wakulima wa
Mikoa ya Ruvuma, Lindi na Mtwara kwa kuwafanya kukielewa kilimo chenye tija.
Mkulima mwingine, kutoka Kijiji cha Chemchem Wilaya na
Nachingwea, Issa Bakari amesema TARI imekuwa mkombozi kwa wakulima wengi katika
kandahiyo kwani imesabisha uzalishaji wa
mazo yao kuongezeka hususani maeneo ya vijijini.
Mimi natoka Kijiji cha Chemchem wilayani Nachingwea
mkoani Lindi nimekuja mahususi katika Banda la TARI ili niongeze uzoefu kutoka
kwa wataalam wabobezi ambao wamekuwa ni msaada mkubwa sana kwetu hasa sisi
wakulima wa vijijini,” alisema Bakari.
Mtafiti wa mbegu bora ya mihogo, Ndwasi Gambo (kushoto) akiwaelekeza wananchi kuhusu kilimo chenye tija za zao hilo. |
Muonekano wa mikorosho kwenye maonyesho hayo |
Mtafiti Msaidizi wa zao la Karanga na alizeti, Said Ally, akielekeza kuhusu kilimo cha zao hilo. |
Mtafiti Msaidizi na Msimamizi wa Kituo Kidogo cha Manyoni mkoani Singida, Eunice Kachungwa (wa pili kushoto), akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda la TARI. Kulia ni Mtafiti Msaidizi wa zao la korosho, Nora Manfield.
Mtafiti Msaidizi wa zao la korosho, Kelvin Kawonga (kulia) akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda la TARI kwenye Maonyesho hayo.
Mtafiti wa mbegu bora ya mihogo, Ndwasi Gambo (wa pili kulia) akiwaelekeza wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama Mkoa wa Mtwara kuhusu kilimo chenye tija za zao hilo. Kulia ni Mtafiti wa zao hilo, Benedetha Kimata kutoka TARI Naliendele.
Wananchi wakipata maelezo ya kilimo bora cha zao la ufuta.
Mtafiti wa Hali ya Udongo na Agronomia ya korosho, Zawadi Kilingala, akielezea kuhusu kilimo hicho.
Mtafiti Msaidizi wa zao la korosho, Dantish Leonard (kulia) akielezea kilimo hicho.
Muonekano wa shamba la ufuta kwenye maonesho hayo.
Muonekano wa shamba la alizeti kwenye maonesho hayo
Muonekano wa shamba la Mtama kwenye maonesho hayo.
Mtafiti wa zao la Korosho, Kasiga Ngiha (kulia) akiwaelekeza wakulima kutoka Wilaya ya Nachingwea, Joackim Lihundi (kushoto) na Bakari Pilipili (katikati) kuhusu mbegu bora za zao hilo.
Muonekano wa kitalu cha mbegu bora za korosho.
Wananchi wakiwa ndani ya banda la TARI Naliendele kwenye maonesho hayo.
0 comments:
Post a Comment