Mnufaika wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF ambaye ni msomi wa Shahada ya kwanza ya masuala ya maendeleo ya jamii Lightness Mwasano ambaye ni mkazi wa Kata ya Kalobe mtaa wa Majengo jijini Mbeya akipanga mikeka yake katika banda la TASAF kwenye maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
***************
1. Ni TASAF usipime, kazi
inatufanyia,
Matunda yake tusome, tuzidi
kufurahia,
Mfuko huu uvume, jinsi
unasaidia,
Lightness Mwasano, yake
yanatuingia.
2. Alikuwa na wazazi, ambao
lijivunia,
Baba kapata makazi, kifo
kilipomjia,
Huku mama hana kazi, TASAF
ikaingia,
Lightness Mwasano, yake yanatuingia.
3. Sana imesaidia, tuko
alikoanzia,
Elimu kumlipia, ngazi
akijipandia,
Mara mama yake pia, kifo
kikamwangukia,
Lightness Mwasano, yake
yanatuingia.
4. Pasipo hii TASAF, yeye
kumsaidia,
Asingezivuka safu, pazuri
akafikia,
Yeye nasi twaisifu, yale imemfanyia,
Lightness Mwasano, yake
yanatuingia.
5. Na wadogo zake pia, TASAF
yasaidia,
Maisha wanapitia, adha
yawapunguzia,
Hapahapa Tanzania, mfuko
twajivunia,
Lightness Mwasano, yake
yanatuingia.
6. Elimu alofikia, shahada
nakuambia,
TASAF afurahia, ilivyomsaidia,
Kero kumpunguzia, ushuhuda
atwambia,
Lightness Mwasano, yake
yanatuingia.
7. Huyu ni mmoja mtu, TASAF
ajivunia,
Wako wengi wengi watu, kwenye
yetu Tanzania,
Tasaf mefanya vitu, wote
wanashangilia,
Lightness Mwasano, yake
yanatuingia.
8. Kazi ni maendeleo, kwa watu
wa Tanzania,
Hakuna upendeleo, Mfuko
wafwatilia,
Kuna mengi matokeo, wale
wanautumia,
Lightness Mwasano, yake yanatuingia.
9. Serikali za Mitaa, zidisha
kusaidia,
Huko kwenu mnakaa, watu
mwawaangalia,
Wahitaji wachakaa, TASAF yasaidia,
Lightness Mwasano, yake
yametuingia.
10. Wanyonge kusaidia, dini
safi nakwambia,
TASAF twashangilia, ndivyo
inatufanyia,
Hongera twawapatia, mnatukuna
sikia,
Lightness Mwasano, yake
yametuingia.
11. TASAF toka zamani, vyema
inatufanyia,
Mfano bora nchini, matunda
twajipatia,
Heko na Serikalini, misuli
kuipatia,
Lightness Mwasano, yake
yametuingia.
Na Lwaga Mwambande (KiMPAB)
lwagha@gmail.com 0767223602
Asante sana
ReplyDelete