Nafasi Ya Matangazo

September 24, 2021

Mwandishi wa ITV na Radio One mkoa wa Songwe, Gabriel Kandonga (pichani) amefariki kwa ajali alfajiri ya leo akiwa njiani kuungana na kamati ya bunge inayoshughulikia masuala ya Ukimwi na Dawa za Kulevya ambayo inaendelea na ziara yake wilayani Songwe.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Omar Mgumba amethibitisha kutokea kwa Ajali hiyo na kusema Marehemu alikua akiendesha gari dogo na alipata ajali kwa kugongana na Lori eneo la Mlowa Tunduma. 

Mgumba amesema chanzo cha ajali kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo ni mwendo kasi.
Posted by MROKI On Friday, September 24, 2021 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo